Heinz Consulting
Member
- Jun 21, 2021
- 10
- 14
Fundraising Event kwenye kwa nchi nyingi, imekuwa na mafanikio makubwa. Matukio haya yamekuwa yakiyawezesha mashirika mablimbali kama vile hospitali, vyuo, asasi za kiraia n.k kukusanya rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi na programu mbalimbali. Waandishi wengi wamejaribu kuchambua aina tofauti za “fundraising events” ambazo shirika linaweza kuzitumia, lakini aina ambazo hutumiwa mara nyingi na mashirika ni hizi zifuatazo;
- Reception: Hili ni tukio ambalo hufanyika kwa wahudhuriaji kupatiwa vinywaji na buruidani au wakati mwingine vinywaji na buruidani vinaweza visiwepo kutokana na ufinyu wa bajeti. Matukio ya namna hii hufanywa sana na taasisi za sanaa kwa ajili ya maonyesho ya kazi mpya zinahusu sanaa.
- Meals: Tukio hili mara nyingi linalenga watu wazima. Watu hawa hukusanywa kupitia mlo wa mchana au jioni (luncheon or dinner affairs) kwa lengo la kushukuru mchango wao kwa shirika husika.
- Participating Event: Hili ni tukio linalohusisha mashindano ya kukimbia n.k (runs, jog-a-thons, walkathons, etc) na washindi wanapata zawadi au vikombe. Matukio haya hufanyika kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa jambo kwa ajili ya wanufaika wa huduma za shirika husika (cause). Ili kuhakikisha ushiriki unakuwa mkubwa, vyombo vya habari kama vile TVs, radio, mitandao ya kijamii n.k hutumika kwa ajili ya uhamashishaji kwenye ushiriki wa tukio hili.
- Community Mega-Events: Haya ni matukio ambayo hufanyika kwa kipindi cha muda mrefu kidogo na huendeshwa na kikundi cha jamii fulani kwa lengo la kusherehekea matukio ya kihistoria n.k. Ili kufaidika na matukio ya namna hii, mashirika ya kijamii nayo huweza kushiriki kama wageni.
- Kukusanya fedha (fundraising). “Fundraising event” inayofanyika kwa sababu hii, inatoa fursa kwa washiriki wa tukio kutoa fedha (monetary gifts) kwa ajili ya kufadhili mradi au programu maalum kwa ajili ya shirika. Ukusanyaji wa fedha kwa njia hii, mara nyingi huwa na gharama kubwa kuliko kiasi cha pesa kinachokusanywa. Kwahiyo mashirika yanapaswa kuwa makini kwenye mipango na utekelezaji.
- Kuwatambua wafadhili watarajiwa (Identifying prospects). “Fundraising Event” inayofanyika kwa lengo hili huwavutia watu wenye maslahi (interests) na shirika ili waweze kuwa wanachama wa shirika ambapo wataweza kuwa wanachangia “cause” mbalimbali za shirika, mfano wa tukio hili ni gala n,k
- Kutoa elimu juu ya shughuli za Taasisi na kusajili wafadhili wapya (Education and cultivation) “Fundraising event” inayofanyika kwa sababu hii, hutoa elimu juu ya programu mbalimbali zinazofanywa na shirika husika. Matukio ya namna hii huongeza mvuto wa shirika kwa jamii pia hupelekea kukubalika kwa “case for support” ya shirika kwa jamii.
- Kutambua mchango wa wafadhili na wadau wengine (recognition) "Fundraising event” inayofanyika kwa sababu hii, hutambua michango ya wafadhili mbalimbali ambao wamewahi kulifadhilli shirika hapo awali, pia kutambua mchango wa watu wanaojitolea (voluntarism) kwenye shirika ili kuwatia moyo.
Article By;
HEINZ Management Consulting
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
P.O Box 12119
Dar es Salaam
For Consultation Service; Call +255 719 518 367 or
Email: heinzconsultancy@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania