Aina ya biashara waweza kuanzisha kwa mafanikio

Jumaa gosso

Senior Member
Sep 4, 2016
188
127
AINA YA BIASHARA WAWEZA ANZISHA
KWA MAFANIKIO:
Biashara na dunia ya digitali yahitaji mengi maarifa ya kuwekeza ili kukubakisha katika mfumo ,nimeshuhudia mamia ya watu wakirudi
katika umasikini ulio kidhiri lakini hapo awali walikuwa na biashara kubwa tu za maana,dunia ya sasa yahitaji kufikiri kwa haraka ili ufanye maamuzi sahihi ndani ya muda mfupi,kama ukikosea kufikiri vema mfumo unakutupa nje,

Biashara ya karne hii zipo za aina mbili bidhaa na kutoa huduma,hizi
zote zinahitaji uwekezaji mkubwa wa maarifa, huduma huhitaji mtaji mdogo sana wa maarifa na huwa inalipa kwa kiasi kikubwa ,mathalani
idadi kubwa wa matajiri duniani hutokea kwa huduma mfano Helu slim,Bill gates Michael dell na wengi sana ni huduma,

Japo bidhaa inalipa sana sema inahitaji kuwekaza zaidi kuliko
huduma pia zote huduma na bidhaa zinahitaji mtu awe na malengo ili uweze kudumu,katika ukanda wa afrika mashariki kuna aina mbalimbali zinazoendeshwa lakini swali kuu ni je hizi biashara huwa zinadumu baada ya
miaka mitatu au zinakufa?

kabla ya kujengwa kwa mlimani city barabara ya sam nujoma na
kutoka mwenge kwenda posta kulikuwa na maduka na baa nyingi je leo ukipita zipo?mara nyingi biashara nyingi huanzishwa pasipo malengo,dira na maono kamili nyingi hutokea kwa sababu Fulani kafanikiwa basi mwingine huenda kuwekeza sekta hiyo ,katika dunia ya sasa kuna aina zifuatazo kuu za biashara:

(i) Biashara ya asili(traditional business) hii ni biashara ambayo imezoeleka miongoni mwa wengi sana sana wazawa,katika hii mtu anakuwa na mtaji na kufungua biashara yake baada ya kufuata mlolongo wa kuandikisha
biashara yake,mfano wa hizi biashara ni baa,biashara ya daladala nchini,biashara ya maduka,nk.

Hii aina ya biashara ni maarufu sana miongoni mwa wanajamii ,mara nyingi
ipo sana sana ipo maeneo ya wanapotokea watu wa tabaka la tatu na la pili,hapa ndipo kwenye walipa kodi wengi ukiachilia mbali
wafanyakazi.

Sifa kubwa yah ii aina ni ina aina ya usambazaji wa mlolongo kutoka
kiwandani,kwenda kwa wauzaji wa jumla,rejareja na hatimaye mtumiaji.

(ii) Biashara kutumia jina la kampuni kubwa duniani kibiashara (franchises), makapuni mengi hapa nchini ni yakununua brand name ya
kampuni kubwa ya nje na kulitumia katika biashara baada ya kukidhizi viwango vya kampuni husika,mfano Tanzania kuna kampuni za cocacola,steers restaurant,mc Donald, the guardnian, dasani, daily news, ITV, nk

Hizi zote zimenunua majina ya hizi kampuni baada ya kufikia viwango vya kampuni husika,sifa kubwa ya hizi biashara unatakiwa uwe na mtaji mkubwa maana unatakiwa ulipe kodi (loyality) kwa kampuni mama au kwa lugha, uchangie gharama za matangazo kwa kueneza kwa gharama yako haya matangazo kutoka nje na jina nzuri(goodwill).Pia siku hizi kampuni nyingi zinafanya kujisajili kwa kampuni kubwa (affiliation) .

(iii) Biashara za mitandao(networking market), hii ni ndoo biashara iliyoibuka miaka ya sasa hivi Afrika ,japo ilikuwepo toka miaka ya 1940’s
maeneo ya nchi za magharibi ,wanazuoni wengi wametabiri ndio biashara ya karne hii baada ya kuondoa zile gharama za utangazaji katika ya mzalishaji na mtumiaji,

Hapa inakuwa muuzaji ndio mteja na kadri anavyoleta wateja
wengine analipwa kulingana na idadi na hiyo idadi ikileta wateja wengine hawa wote watahesabika ni Yule wa kwanza ,na wale waliwaleta wengine watalipwa kwa hiyo idadi,mfano A ameleta B ,C,na D basi A atalipwa kwa gharama za matangazo za kuwaleta B,C na D maana hii itatumika kama vocha ya A kulipwa

Mathalani B,C na D wakaleta wengine E,G,H,I,J,K hapa A atalipwa
kwa gharama za wote hawa kupitia vocha za B,C na D,na pia B,C na D watalipwa kwa vocha za E,G,H,I,J,k nao hivyo hivyo kwa hawa kama
wakileta watu na kuwa wateja na wauzaji huu wote ni mtandao unakuwa na kusonga mbele sifa kuu wale waliowahi ndio watanufaika sana.

Biashara za kileo zahitaji ubunifu,na maarifa mengi hivyo umakini wa kuchagua
wapi uangukie unatakiwa umakini sana,biashara za mitandao ni nzuri sana, kwani kadri mnavyokuwa wengi kunufaika na kuzidi kuimarika hivyo kuwa biashara ya kileo.
 
Back
Top Bottom