Mazingira Ni pamoja na shinikizo la wazaz, msichana kutegeshea kupata mimba bila kijana kujua, umri kuwa mkubwa pasipo kuoa au kuolewa, mwanamke au mwanaume kufata mali ya mwenza nk, chunga sana kuingia kwenye ndoa za shinikizo,
Ya kwanza: Ni ile mwanaume kampenda mwanamke na kaona njia rahisi ya kuendelea kuwa karibu na mwanamke huyo ni kumuoa. Na mwanamke kwa kulazimishwa na mazingira anakubali kuolewa.
Ya pili:Ni ile mwanamke anampenda mwanaume na kaona njia rahisi ya kuendelea kuwa karibu naye ni kumganda mpaka aolewe. Na mwanaume kwa kulazimishwa na mazingira anaamua kuoa.
Ya tatu na ya mwisho: Ni ile mwanaume na mwanamke wote wamependana na wameamua kuoana na kuanzisha familia.
Sasa hizi ndoa mbili za mwanzo ndo zinafanya wanaume walio wengi walee watoto wasio wao, maana mwisho wa siku mwanaume au mwanamke bado atahitaji kuchepuka ili kujiridhisha.!!!!
Tujadili kwa uwazi.
Kama ni mwanaume na unahisi ndoa yako inaangukia kundi la kwanza au la pili basi nakushauri ujiwekee utaratibu wa kupima vinasaba(DNA) kila ukibahatika kupata mtoto!!!!!!!
Nawasilisha
Hapo kuna msukumo wa umri, uchumi, na msukumo wa wazazi na vitu vingine vingi tuu
Naomba ndoa yangu iangukie type number 3 Amen
Mazingira Ni pamoja na shinikizo la wazaz, msichana kutegeshea kupata mimba bila kijana kujua, umri kuwa mkubwa pasipo kuoa au kuolewa, mwanamke au mwanaume kufata mali ya mwenza nk, chunga sana kuingia kwenye ndoa za shinikizo,
Hapo pa kulazimishwa na mazingira hapo,nasubiri ufafanuzi!!!!
Mazingira yanilazimishe kuolewa na mtu nisiyempenda!!!!
Hayo mazingira ni katili sana
Naomba ndoa yangu iangukie type number 3 Amen
wanawake hufikia hatua ya kudaka mimba ili aolewe,wasichana wengi siku hizi wanaolewa wakiwa wamewezeshwa tayari(wanamimba)