Aina mpya ya utapeli

Dah jamaa inaonesha ana imani za kipuuzi sana.

Hapo kwenye mzizi tu ilikuwa aweke dault,naamini uchawi upo ila amepigwa kizembe

Jamaa akaundiwa tume huru ya utapeli 😀😀😀
Hiki ki-ebrania nini mkuu?🤣
 
Wahuni Wakamtengeneza Siku Hizi Wizi Wa IT Ndiyo Huo Sasa
Science And Technology
 
Kwa simulizi hii bado unamwita mlokole mshamba!!🤔
 
Hii sio ngeni, labda kwako wewe
 
Kuna mwandishi anaitwa Harlod Atu kaandika kitabu kinaitwa "MBINU ZA MATAPELI" kisome hicho kitabu ujifunze kitu, unaweza jikuta unaanza kuwa mpigaji, Nakala kibao za kitabu hicho zilichomwa moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao jamaa wamesoma aisee
 
Hahahahaha walai nacheka kama mazuri,
Jamani eeh tukubali tukatae huwezi kutapeliwa kama huna Tamaa, wengi husema Matapeli wanatumia dawa, jibu ni HAPANA, Matapeli wanakutapeli kwa tamaa yako yaan wao hukutia tamaa ukitamani tu wanakuchinjia baharini,

Hao washenzi walishakuja dukani kwangu mara ya mwanzo walimkuta binti, wakamjaza kwa kudai kua rangi nyekundu niliyopaka sio ya biashara, nakosa wateja wanaostahili sababu ya rangi, basi sijui walimwambia na mengine yapi binti ananipigia simu kahamanika anataka nibadili rangi haraka nikamwambia atulize pupa kwanza sina pesa za kuchezea akasema eti nikate kwenye pesa yangu hapo nikahisi binti amechanganyikiwa nikamtuliza akatulia,

Sasa siku hiyo nakumbuka ilikua jumamosi nimekaa zangu dukani na ndugu yangu tunasogoa akaja libaba refu jeusi akajiulizisha kitu nikawa sina akadai alimuagiza binti amuwekee nikamwambia sijapata hiyo order, akaanza, "wewe ndie mmiliki wa hili duka?? Hii rangi unaijua maana yake??? Hiyo ni rangi hutumiwa na waganga na wachawi, hupati wateja unaostahili sababu tu ya rangi, nimeona shetani nani sijui ametawala dukani kwako...." Akaongea blah blah kibaoooooo mwisho wa siku akadai anipe dawa ya kudekia saa 11 alfajiri, nitashangaa wateja watakavyokuja, nikamuuliza bei gani hiyo dawa akasema elfu 2 tu ila majibu yatakavyotokea nitajua mwenyewe nimpongeze kiasi gani,

Tangu mwanzo nilishanusa harufu ya utapeli nikamwambia aache namba nitampigia, akaanza kulazimisha ooh nakusaidia, ooh fikiria nimeacha maduka mangapi hadi nimekuja kwako, mimi nakupa dawa uwe tajiri, hapo nikajiaminisha kua huyu kama sio Tapeli basi Jambazi kabisaaaaaa,

Nikamwambia atoke haraka kabla sijamuitia mwizi, akaondoka ila nikasikia kuna Mmama alifilisiwa na huyo huyo jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…