Aibu ukweni leo

jogijo

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2019
Posts
262
Reaction score
509
Habari wadau,
Leo nilikimbia kidogo ukweni kusalimia wazee wangu walionizalia mke wangu mzuri.. Baada ya kupiga story na kupata msosi tukaanza kufunga mizigo (ya kumletea mtoto wao nyumbani) wakata kuku wawili jogoo na jike wanakimbizana, bahata nzur kufika pale jike akakosa njia na jogoo likaanza kazi.
Aibu imekuja hapa, ni nani asimame amfukuze awafukuze? Mimi nikavunga na baba mkwe kavunga, mama mkwe kasimama kwenda kuwafukuza ila anapiga hatua akatereza akaanguka... mimi nilikosa cha kusema na baba mkwe akakosa cha kusema yaan tukakaa tumetazamana tu.
Mila zetu haziruhusu kijana kumgusa mama mkwe ningeenda kusaidia, ashukuriwe Mungu baba alikuwepo.
 
Duh likitokea tukio la hivyo siku nyingine kausha kama haupo... mkiwafukuza ndio aibu inakuja..

Au kama mnacheki movie ikaja scene ya kupigama denda usifoward... wewe kausha kama mbuzi tu..
 
So mfano hata Baba mkwe hakuwepo wala hao kuku.

Ikatokea upo afu Ma mkwe akashikwa na kifafa kwa mfano. Ama she just loses consciousness.

Ina maana utamuangalia tu?

Hizi taboos ndo sasa huwa zinapelekea watu kufika kwenye kuonja forbidden fruits.

Hazina maana.
 
Samahani, sikukosei heshima Mkuu; ila wote, wewe na wakwe wako, mnawaza uchafu.
 
Unaaribuje starehe ya hao Ndege ikiwa wao hawajawah kukusumbua ukifanya yako..... Naonga hoja Mama mkwe angetoka jino.
 
ungemnunulia hata pipi mama mkwe ili apunguze maumivu
 
Hata nature watu wanataka kuingilia kisa kulinda MILA ZAO!!! Huyo mama angeweza hata kuvunja mguu kisa kuwazuia kuku wasifanye tendo la AIBU! 😏😏😏

Kisa cha kuwafukuza hao kuku ni nini? Nyie nani huwa anawafukuza?
Ni wivu tu.
 
Sioni ubaya ikiwa umedumisha MILA yako
 
Hata nature watu wanataka kuingilia kisa kulinda MILA ZAO!!! Huyo mama angeweza hata kuvunja mguu kisa kuwazuia kuku wasifanye tendo la AIBU! 😏😏😏
Si ndio hapo sasa!!
 
Reactions: BAK

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…