ULUMI
Member
- May 25, 2011
- 70
- 37
Nina masikitiko ya kutosha kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa namna ambavyo limeshindwa ku handle mgogoro wa Junior Seminary Morogoro kufikia hatua ya kuwarudisha nyumbani wanafunzi wote baada ya mgomo wa kutaka uongozi wa shule hiyo ubadilishwe. Madai ya wanafunzi hayakupewa nafasi ya kusikilizwa licha ya kwamba ni mara ya pili kuzuka mgogoro shuleni hapo.
Kwanini nasema ni aibu TUPU kwa KKKT; Kwanza naamini kabisa kuwa waumini walio wengi wanapeleka wanafunzi wao katika shule zinazoongozwa na Kanisa la Roman Catholic. Ambazo zilizo nyingi zinaongoza kwa kufanya vizuri katika masomo pia wana uongozi mahiiri wa usimamizi wa shule zao.Licha ya kwamba zinaongozwa na mashirika ya Kikanisa lakini msingi wake ni mmoja tu MAADILI MEMA.
Swali langu kwa Kanisa la Kilutheri kwanini shule zake hazifanyi vizuri ukilinganisha na Roman? Na Je uongozi wa juu hawaoni haja kubwa kutilia maanani ELIMU kwanza kuliko hata ujenzi wa mahekalu na vitega uchumi ? Ambvyo wame excel kwenye kukusaya michango?
Sina nia ya kulaumu KANISA bali uongozi wa juu unapaswa kutilia maanani zaidi katika kuimarisha shule zake zilizopo hata na kuanzisha zingine nzuri zaidi ili kuleta ufanisi zaidi.
Najaribu kuelewa kuwa migogorop mingi kwenye shule zetu hasa ni upungufu wa mahitaji ya msingi,kama vile Uongozi usio kidhi matakwa ya Elimu,maadili mema,miundombinu nk nk.
Najisikia aibu sana mimi mwenyewe nikiwa muumini wa Kanisa hilo pale naenda kupanga foleni katika shule za Roman Catholic kupata nafasi ya mtoto ili hali sisi tunao uwezo wa kuboresha shule zetu na hata kushindana na hawa wenzetu,Tena basi kwa mtizamo huo huo naliona KKKT kama lina wasomi wengi wazuri na viongozi wenye upeo mpana sana.Je hili la Elimu linatupigaje chenga?
Jana watoto walirudishwa majumbani wakiwa wengine hawana hata nauli ya kurudi makwao wala mawasiliano na wazazi wao, kwani wametoka likizo siku si nyingi tuu.Mheshimiwa Baba Askofu Dr.Alex Gehaz Malasusa angalia jambo hili kwa makini kanisa lina matarajio mengi sana kwako katika hili. UBARIKIWE NA BWANA.