Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Nimepata fursa ya kwenda kumpa mkono wa Krismasi ndugu yangu,rafiki yangu, Kiongozi mwenzangu katika Chama,mpambanaji mwenzangu Kamanda Godbless Jonathan Lema anayeendelea kusotea haki yake katika gereza la Kisongo Mkoani Arusha.
Nimefarijika sana kwa hali niliyomkuta nayo kiafya na kiakili, bado ni mwenye afya njema sana,ucheshi na uimara wa hali ya juu katika misimamo yake kifikra na kimtazamo.
Namuona Lema akizidi kuimarika kifalsafa na kimsimamo kwa yale yote ambayo amekuwa akiyaamini na akiyatamani kwa Chama chake na nchi yake Tanzania. Jambo hili linanifurahisha sio kwamba napenda kumuona rafiki yangu akiendelea kusota rumande hapana kwa sababu najua maisha ya gerezani,nimeyaishi bali nafurahi kuona nafsi yake ikikataa kuingia katika mtego wa watesi wake wa kumkatisha tamaa na kumrudisha nyuma katika azima na ndoto yake ya kulipigania taifa lake.
Hii ni mara ya tatu kwangu kufika gerezani Kisongo kumjulia hali rafiki yangu Lema tangu alipoingizwa katika gereza hilo nkiwa na lengo la kumfariji.kumtia moyo na kumuonesha kuwa tulio nje tunatambua na tunaheshimu dhamira yake njema ya kulipambania taifa lake.
Natambua kuwa na yeye angetamani sana kuwa nje kusherehekea Krismasi na familia yake, haikuwa hivyo, sio kwa kupenda bali ni matokeo ya ndoto kuu aliyonayo kuhusu taifa lake kwa masilahi mapana ya watoto wake na watoto wa wenzake kwa gharama kubwa ya maisha yake watoto wake, mke wake na wazazi wake.Ni kwa hekima hizo nami niliamua kutokula Krismasi na familia yangu!
Nataka Lema ajue na hata watesi wake wajue kuwa anachokisimamia Lema ni ndoto ya wengi, tutaumizwa,tutateswa,tutapotezwa,tutafungwa lakini tuna amini kuwa tunatimiza wajibu wetu, hatumdhulumu mtu wala kumuonea mtu,haki na demokrasia tunayoipigania ni sehemu ya wajibu wetu kwa nchi yetu.
Wengi wamesherehekea Krismasi na familia zao, wakila na kunywa kwa furaha wengine wakina Lema wamekula Krismasi gerezani mbali na familia zao ikiwa na matokeo ya kutetea wengine ili waishi vizuri. Kazi hii haihitaji ahsante wala bakshishi,hakuna fidia yoyote yenye kukidhi malipo stahiki, ni kazi ya kujitoa muhanga ili wengine waishi vizuri,ni kazi inayohitaji uzalendo wa hali ya juu, ni kazi ambayo haina fidia yoyote kulipa gharama ya maisha na hatari ya maisha mtu anayoibeba kwa faida ya wengine, malipo yake ni kwa Mungu tu aliyeamua kuchagua wachache kupigania haki za walio wengi.
Ahsante sana Kamanda Lema kwa kuonesha ukomavu na ujasiri katika kusimamia unayoyaamini, niliwahi kuandika mwanzoni kabisa ulipotoa maono yako kuwa Mungu alikuchagua wewe kwa kuwa alijua kuwa hutoogopa kuwasilisha ujumbe na kwamba walengwa badala ya kukaa na kutafakari kwa kina maono yako kwao wao njia pekee watakayoiona ni bora ni kukushughulikia wewe, unanipa faraja kubwa sana kila ninapokuja gerezani unapooonesha kujiamini na kunipa ujumbe mzito kuhusu harakati zetu,najua hutosoma ujumbe wangu huu usiku huu lakini naamini salaam zitakufikia, unanifariji sana na ninatilia maanani kila neno na kauli yako kwangu kuhusu Chama chetu na harakati tunazoziendesha na mazingira yake.
Nakupenda sana, na kwa kuwa kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho naamini hata lako hili lina mwisho. Mungu akulinde na akuzidishie ulinzi,afya njema,hekima, busara na mapenzi yasiyoyumba kwa nchi yako.
Ahsante kwa Neema mkeo, ni wazi kwa kila anaemuona Neema alivyo madhubuti na kuhimili vishindo unavyopitia wewe mumewe na kubakia imara ni dhahiri watakubaliana nami kuwa ipo siku vitabu vya historia ya nchi hii vitaandika jina lake kwa wino wa dhahabu.
Mungu Ibariki Tanzania
Aluta Kontinua
Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
Chadema
25/12/2016