Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,442
- 33,999
- Thread starter
-
- #21
Vito...Mkuu, lakini hao wamakonde walipofika Zanzibar,.... Waliongozwa na John Okello kwenye Mapinduzi .. . Okello ndio alikuwa front line kwenye mapambano....Halafu hicho kitabu nasikia kilipigwa marufuku.
Hapo sasa tutaenda sawa,. .... nieleweshe rolle ya John Okello, Kassim Hanga kwenye mapinduzi Zanzibar?. Na kwanini Okello alifukuzwa Zanzibar?Vito...
Ungekuwa mjanja na unataka kuelimika ingekuwa mapema ushatambua kuwa unajadiliana na mjuzi anaeifahamu vyema historia ya mapinduzi.
Usingekuwa unajifanya kujua ilhali huna moja ulijualo.
Sasa nakupa nafasi ya kuuliza maswali nikufunze historia ya mapinduzi.
Hiyo picha hapo chini niko katika ufukwe wa Kipumbwi wakati wa utafiti kuliangalia pori la mafunzo na sehemu majahazi yaliyokuwa yakiwavusha Wamakonde yalipokuwa yakiegesha nk. nk.
Unasema kitabu kilipigwa marufuku.
Kilipigwa marufuku lini ilhali hata hicho kitabu hakijafika nchini?
Kwa nini huandika mambo unayoyajua?
View attachment 2247059
Vito...Hapo sasa tutaenda sawa,. .... nieleweshe rolle ya John Okello, Kassim Hanga kwenye mapinduzi Zanzibar?. Na kwanini Okello alifukuzwa Zanzibar?
Kitabu kilopigwa marufuku ni 'Ukweli ni huu'Mkuu, lakini hao wamakonde walipofika Zanzibar,.... Waliongozwa na John Okello kwenye Mapinduzi .. . Okello ndio alikuwa front line kwenye mapambano....Halafu hicho kitabu nasikia kilipigwa marufuku.
Angel,Kitabu kilopigwa marufuku ni 'Ukweli ni huu'
Nishamsahau muandishi
Kwaheri Uhuru ,Kwa heri ukoloni nacho kimepigwa marufuku.... Said Mohamedi ni ubishi tu, hapendi kusikia mambo asiyoyapendaKitabu kilopigwa marufuku ni 'Ukweli ni huu'
Nishamsahau muandishi
Vito...Kwaheri Uhuru ,Kwa heri ukoloni nacho kimepigwa marufuku.... Said Mohamedi ni ubishi tu, hapendi kusikia mambo asiyoyapenda
John Okello umemsahauVito...
Huijui historia ya mapinduzi.
Mipango ya kuipindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte ilikuwa inaratibiwa Tanganyika na iliwekwa kambi Kipumbwi, Tanga ambako Wamakonde kutoka Shamba la Sakura walikuwa wakipewa mafunzo.
Wasimamizi wa kambi hii walikuwa Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe Regional na District Commissioner wa Tanga.
Wengine waliokuwa katika mpango huo katika kuwatafuta Wamakonde watakaovushwa kwenda Zanzibar walikuwa Victor Mkello kiongozi wa wafanyakazi wa mashamba ya mkonge na Mohamed Omari Mkwawa.
Huyu Mkwawa yeye ndiye aliyekuwa akiwavusha hawa Wamakonde usiku katika majahazi wakijifanya wavuvi na kuwafikisha Zanzibar.
Waliokuwa wanasimamia mipango hii walikuwa Oscar Kambona na Abdallah Kassim Hanga.
Unaweza kusoma historia hii kwa ukamilifu katika kitabu hicho anachokionyesha Mohamed Omari Mkwawa hapo chini:
View attachment 2246675
Uzalendo,Jo
John Okello umemsahau
Kwaheri Uhuru ,Kwa heri ukoloni nacho kimepigwa marufuku.... Said Mohamedi ni ubishi tu, hapendi kusikia mambo asiyoyapenda
Mzalendo...Shukrani na pongezi za kipekee ziende kwa Mkombozi na Shujaa wetu aliyetuletea Uhuru, amani, Upendo, Umoja na Mshikamano Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Maelezo haya hayaniingii akilini.... Hahahahaaa, eti alitumika kutisha watu... Ili wakubali mapinduzi....Vito...
Katika kitabu cha Harith Ghassany, "Kwaheri Ukoloni...'' (2010) Okello anaelezwa kama mtu aliyetumika kutisha watu kupitia radio kwa kutangaza mapinduzi.
Alitakiwa kwa ile lafidhi yake ili Wazanzibari wawe na fikra vichwani mwao kuwa nchi imevamiwa.
Alivikwa blanketi kama inavyoelezwa ajione yeye ni mtu muhimu kwa kuwekwa mbele ili ikiwa patatokea lolote la mapinduzi kushindwa yeye ndiye atiwe hatiani.
Khamis Abdalla Ameir (2022) anamtaja John Okello kama mtu msumbufu aliyetaka kujitia kila mahali na kuwa bughudha akitoa maneno ya ovyo hadharani.
Hii ndiyo sababu akafukuzwa Zanzibar.
Ama kuhusu Kassim Hanga yeye nimekwisha kumueleza.
Kapu...Maelezo haya hayaniingii akilini.... Hahahahaaa, eti alitumika kutisha watu... Ili wakubali mapinduzi....
Na alivikwa blanketi... La utiisho!!!!
Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
Habari Mzee,Kapu...
Kuamini au kutoamini hii ni khiyari yako hakuna wa kukulazimisha.
Mimi nimeshiriki katika utafiti wa mapinduzi na nimefika hadi Kipumbwi ilipokuwa kambi ya Wamakonde na nimeshihudia kote kulikohusishwa na mpango huo.
Nimesikiliza mahojiano baina ya Dr. Harith Ghassany na Mohamed Omari Mkwawa ambae Mzee Karume alimpa jina la Tindo wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar.
Mkwawa ndiye aliyetufikisha Kipumbwi na nyumbani kwa Victor Mkello, Nguvumali Tanga.
Huyu Mkwawa hakupata kufungua kinywa chake kwa mtafiti kabla ya Dr. Ghassany.
Nimesikiliza mahojiano ya Dr. Ghassany na Victor Mkello kuhusu Kipumbwi.
Huyu pia alikuwa kimya miaka yote.
Kuna watu hadi leo hawakubali kuwa kuna Wamakonde walivushwa kuingia Zanzibar 1961 kupigia kura ASP na 1964 kusaidia mapinduzi.
Sishangai kuwa wewe huamini haya niliyokueleza kuhusu John Okello.
Nitashangaa ikiwa utakuwa unaamini John Okello alikuwa Field Marshall.
Richard...Habari Mzee,
Kabla ya uhuru na hata miaka ya mwanzoni baada ya uhuru Nyerere alikuwa na uhusiano mzuri na Uingereza pia hakuwa mpingaji wa sera za kibepali, nini sababu iliyopelekea Nyerere akabadilika na kuegemea sera za ujamaa hadi kuja na Azimio la Arusha(1967)?