AHMED OMAR; Kikwete, Shein mwaumbuka Zanzibar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
– Sehemu ya Kwanza

Posted on December 1, 2012 by zanzibardaima • Posted in Politics •



Uchambuzi huu wa Ahmed Omar unaangazia hatima ya Maridhiano ya Wazanzibari mikononi mwa Chama cha Mapinduzi ambapo unahojia kwamba ndani ya kundi la wahafidhina wa CCM Zanzibar wakishirikiana na kundi la watawala Dodoma, kuna dhamira ya kuyafelisha Maridhiano hayo na kuuvunja Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Zanzibar Daima inauchapisha uchambuzi kama sehemu ya jukwaa la maoni. Endelea kusoma….

Je, uongozi wa juu wa CCM hauna imani ya kweli na Maridhiano ya Wazanzibari.

Maridhiano ya Wazanzibari hayakutoka Dodoma na kuna kila ushahidi kuwa hayakupata Baraka za Dodoma. Maridhiano ya Wazanzibari hayakutoka kwa wahafidhina, maagenti wa Dodoma walioko Zanzibar na halkadhalika kuna kila aina ya ushahidi sio tu hayakupata baraka zao lakini waliyapinga na wanaendelea kuyapinga kwa nguvu zao zote. Shabaha ya kupinga maridhiano ya Wazanzibari na serikali ya Umoja wa Kitaifa ni kujenga farka, fitna, chuki, ukabila, ugozi, chokochoko na uvunjifu wa umoja na mshikamano miongoni mwa wazanzibari ili kurejesha hali kama ilivyokuwa huko nyuma. Lengo ni kwamba Dodoma (mkoloni mpya wa Zanzibar) aendelee kuitawala Zanzibar na mawakala wao (wahafidhina wa Zanzibar) waendelee kujaza matumbo yao huku wazanzibari walio wengi wakiteseka ndani ya ardhi yao tukufu.


Lengo kuu la mtandao huu wa kupinga maridhiano ni kujaribu mbinu hii na ile ili kuizima nuru njema ya umoja wa wazanzibari ambayo ndio silaha pekee wanayoitegemea hivi sasa katika kuirejesha Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Lengo ni lile lile linaliandaliwa na "system" chini ya watawala wa Jamhuri ya Muungano na vibaraka wao wa Zazibar kuwa wazanzibari wasambaratike, wagombane, wasiwe wamoja, wasiaminiane na wasisikilizane.




Wanamtandao wanafahamu kwamba Wazanzibari wakiwa wamoja wanapata jukwaa la pamoja la kujadili na kusahau mawazo ya tofauti zao za kisiasa na huhisi machungu ya kudhalilika kwa nchi yao. Ukiwaondoa wazanzibari katika maelewano na umoja kwa kujenga mazingira ya kila upande uone bado sisi ni maadui kumbe baina yetu unafanikisha mpango wa kuwagawa katika agenda tunayoipigania.Mbinu kubwa wanayotumia maadui hawa wa Zanzibar hivi sasa ni ile ya kuandaa matukio mbali mbali na kuyanasibisha matukio hayo na UAMSHO kwa upande mmoja na kwa upande wa pili wakifanya kila wawezalo kuziunganisha harakati za UASHO na zile za chama cha CUF na kuziundia harakati zote mbili picha ya uongo zionekane kuwa zipo chini ya mwamvuli mooja na amri moja.

Lakini hebu tujiulize hivi hapa maadui hawa wa Zanzibar wamekuja na staili mpya? Haya ni mambo makongwe kabisa kwa Zanzibar ambayo yameshazoeleka. Kwa lugha nyengine hizi ni propaganda za kitoto kwa wazanzibari, hakuna jipya.Siku ya tarehe 3 Machi 1996, enzi zile wazanzibari walipogawanywa na kutiwa chuki baina yao ilidaiwa na serikali kuwa mafiasa watatu wa usalama waliokuwa kwenye doria huko katika kijiji cha Shengejuu, kisiwani Pemba, walipigwa na kuporwa silaha na wanakijiji. Kwa sura ya kawaida ya uaskari ni vigumu kuaminika kwamba askari watatu wakiwa na silaha mikononi waporwe silaha zao wote watatu na wapigwe bila ya wao hata kujeruhi mtu yeyote au kujeruhiwa wao wenyewe.

Muda sio mrefu, siku ya pili yake tu, kijiji hicho kilivamiwa na kiasi cha askari wapatao 300 wa kikosi cha FFU na jeshi la wananchi (JWTZ) waliokuwa wako kamili kivita. Unyama, mateso na vitendo vya kihuni walifanyiwa wananchi wa kijiji cha Shengejuu. Sio tu unyama huo walifanyiwa washukiwa, lakini pia mateso yaliwakuta watu wengi waliokuwa hawana hatia yoyote. Baadhi ya wanakijiji walipigwa hadi kuzirai, wengine waliibiwa mali zao kama vile kuku na mbuzi, maduka yaliporwa, wanawake walibakwa na watu wapatao 80 waliwekwa ndani.



Kati ya watu hao 80, watu 30 waliachiliwa huru na waliobaki waliendelea kusota ndani kwa kipindi kirefu sana. Kiongozi mmoja mkuu wa SMZ wakati ule, aliwahi kufanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea hali ya mtafaruku inayoendelea katika kijiji hicho cha Shengejuu, na hapa namnukuu moja ya kauli zake aliyoitoa kupitia kikao hicho"Sasa tunataka kuwafanya watu wajue kama serikali ipo".




Katika enzi hizo wafuasi wa CUF walikuwa wakisingiziwa kuhusika na hujuma mbalimbali kama vile kuchomwa moto madarasa ya skuli, kupaka vinyesi kwenye kuta za skuli, kutia vinyesi kwenye visima n.k. Hizi bila shaka zilikuwa ni mwendelezo wa propaganda chafu za kisiasa zilizokuwa na lengo la kujenga picha ya uongo na kuhalalisha hujuma dhidi ya watu wasio na hatia. Waliokuwa wakifanya haya ni watu waliofundishwa vyema propaganda na siasa chafu za uchochezi. Wakitekeleza vitendo hivyo huku wakilindwa na askari polisi.




Madhumuni ni kuendelea kupata fursa ya kuwatesa raia wasio na hatia kwa kuwapiga, kuwaweka gerezani na kuwaua. Waliokuwa wakifanya vitendo hivyo hawakujua kwamba walikuwa wanaonekana na wanafuatiliwa nyendo zao na hivyo kufahamika wao na waliowatuma.




Mkasa wa Shengejuu 1996



Katika hatua nyengine Siku moja wanakijiji hao hao wa Shengejuu katika nyakati za usiku wakiwa katika doria yao ya kuangalia ni nani hasa wanaofanya vitendo hivi, walifanikiwa kuwafumania watu hao. Wakiwa wanaendelea na doria, wanakijiji hao waliiona gari yenye namba za usajili ZNZ-12633 inayomilikiwa na usalama wa taifa ikisimama kiasi cha umbali wa mita 100 hivi kutoka ilpokuwepo skuli ya Shengejuu (Soma kitabu cha Dr. Mohamed Bakari, 2001 kiitwacho The Democratization Process in Zanzibar).



Ghafla watu watatu waliokuwa na galoni la mafuta ya petroli walishuka kutoka katika gari hiyo. Haraka haraka wakamwaga mafuta na kuchoma baadhi ya majengo ya shule hiyo na kukimbia.

Wanakijiji wakajitokeza ghafla na kuwazingira wahalifu hao. Lakini mara milio ya risasi hewani ikasikika na watu hao kuingia ndani ya gari yao na kukimbia. Wanakijiji waliwahi kuuzima moto huo. Ilithibitika kuwa watu waliofanya vitendo hivyo ni wanamaskani waliokuwa wakilindwa na wanausalama ndio waliokuwa wakitekeleza vitendo na hujuma zile kwa nia ya kukizulia chama cha CUF na kuwatesa raia bila ya hatia yoyote kwa maslahi binafsi ya kisiasa.




Wimbi la Mageuzi Zanzibar lawatisha wahafidhina na watawala
Maadui wa Zanzibar baada kuliona wimbi la kudai mabadiliko katika mfumo na muundo wa Muungano wa Tanzania linaongezeka wameamua kujipanga upya na kujaribu kuwasambaratisha wazanzibari ili wasifikie lengo lao kwa kupitia mbinu hizo zilizotumika huko nyuma za kuandaa uongo na kuupandikiza katika jamii. Bila shaka wakitarajia uongo huo utaweza kuzaa chuki na fitna miongoni mwa makundi mabali mbali yaliyoshika kamba ya pamoja kutafuta maslahi ya nchi yao na hivyo kuiwachia kamba hiyo na kusambaratika.


Chuki ambazo zinajengwa hapa ni baina ya CUF na CCM kwa vitendo kama vile vya kuzichoma moto maskani za CCM na kuwasingizia CUF. Kuwatesa wafuasi wa CUF kwa visingizio mbali mbali kama vile kupambana na UAMSHO ili wafuasi wa CUF wakasirike na serikali na chao kwa kuwa CUF ni sehemu ya serikali hiyo. Wafuasi wa CUF wakikasirika dhidi ya chama chao itakuwa tayari umefanikisha kulisambaratisha kundi kubwa linashikilia engine ya kudai mabadiliko na hivyo kuliwacha kundi hilo likiwa dhaifu.Maadui hawa wa Zanzibar wameunda makundi maalum ya uharamia kama vile Ubaya Ubaya, Mbwa Mwitu na mengineyo. Makundi yote hayo yakitoka katika kundi kuu la awali la MAJANJAWIRI. Inaeleweka kwamba janjawiri ni vijana waliochukuiwa kutoka katika maskani za CCM na kupewa mafunzo ya kiaskari kwa lengo la kuajiriwa katika vikosi vya SMZ.

Baada ya kukosa ajira vijana hawa hupewa ajira ya muda ya kufanya hujuma mbali mbali ili kutimiza maslahi binafsi ya chama cha CCM. Hivi sasa majanjawiri wakiwa katika vikosi vipya vya ubaya ubaya na mbwa mwitu wamekuwa wakiratibu na kutekeleza vurugu barabarani, kuchoma moto matairi, na kuchoma moto maskani na makanisa. Halkadhalika vijana hawa ambao ni wepesi wa kuuwa ndio wanaotumika kufanya mauwaji na kisingiziwa vijana wa UAMSHO.Mkasa wa Baa ya Mbawala 2012

Kuna taarifa za uhakika za kikao cha CCM mkoa wa Mjini magharibi kilichosimamiwa na mwenyekiti wake Borafia Silima cha kupanga hujuma za uchomwaji moto wa baa ya Mbawala. Kijana Salim Hassan Mahoja na wenzake watatu wote wakiwa ni MAJANJAWIRI walitumika kushiriki uchomaji moto wa baa hiyo. Kwa kuwa mmiliki wa baa hiyo alijua kua vitendo vya fujo vingeweza kupelekea baa yake kuchomwa, aliomba ulinzi mapema kutoka katika jeshi la polisi.


Askari watatu waliokuwa na silaha bila ya sare walilala katika baa hiyo wakiwasubiri wahalifu pindipo baa hiyo ingevamiwa na kuchomwa. Vijana waliopangwa kuiripua baa hiyo Salim na wenzake walifika katika eneo la tukio usiku na kujaribu kutaka kuchoma moto baa hiyo kama walivyoagizwa. Bahati mbaya askari waliokuwa wamejificha ndani ya baa hiyo waliwashambulia kwa risasi za moto na kijana Salim akafariki hapo hapo huku vijana wenzake wawili wajeruhiwa kwa risasi.



Maiti na majeruhi wote wakapelekwa hospitali ya Mnazi mmoja. Jambo hili limefunkwa halikusemwa wala halikuripotiwa katika vyombo vya habari. Kwa michezo hii ni vipi tusiamini maskani ya KISONGE na nyengine hazikuchomwa kwa mipango hii michafu? Tutaamini vipi askari wa FFU hakuuliwa kwa mipango hii? Tutaamini vipi Sheikh Farid kiongozi wa UAMSHO hakutekwa na mipango hii?



Yote haya yanafanywa ili kuhalalisha hujuma na mateso dhidi ya wana CUF chini ya kisingizio kipya cha UAMSHO baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai kutangaza rasmi katika vyombo vya habari kwamba sasa anataka kupambana na adui yao mmoja mwenye sura mbili, yaani CUF na UAMSHO.



Safu ya Juu ya Uongozi katika hujuma
Kuthibitisha zaidi kuwa serikali ya Muungano na vibaraka wake wa Zanzibar hawana nia njema kwa Wazanzibari na kwamba wao bila shaka ndio wanaoandaa vitendo vya hujuma na vurugu vinavyoendelea Zanzibar ni kikao cha siri kilichofanywa baina ya Rais Kikwete na viongozi wenzake wa Jamhuri ya Muungano kwa upande mmoja na Rais wa Zanzibar na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa upande wa pili.


Kikao kilichoitwa ni cha kuzungumzia hali tete ya Zanzibar kilifanywa na viongozi wa SMT na SMZ huku wakimtenga Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar akiwa ndio kiongozi wa pili kwa ukubwa katika serikali ya Zanzibar. Hii imefanywa kusudi ili kuhakikisha kuwa siri za mipango michafu na hujuma ianyotekelezwa Zanzibar haivuji na kufahamika na viongozi wa CUF kwa kuwa ni dhahiri mipango hiyo wao ndio inayowalenga.Dk. Shein na Kikwete tunakwambieni mufunguke na muache mara moja dhamira zenu mbaya kwa Zanzibar iliyokwisha kujifungua. Tumeugua maradhi ya kugombanishwa miaka mingi na mwisho tuliyapatia dawa. Baada ya kuyapatia dawa maradhi hayo wazanzibari tumefahamu tutakacho, na bila ya kutafuna maneno ni nchi yetu yenye mamlaka kamili.

Wazanzibari tumeapa hatuondoki katika mstari huo. Tunakutahadharisha sisi haturudi nyuma wala hatutetereki tunazidi kushikamana sote tunaohitaji mabadiliko kuelekea mamlaka kamili ya nchi yetu. Wimbi letu ni kubwa sana, nyinyi hamna uwezo wa kulizuia wala kulishinda. Anzeni kutafakari kabla ya hayajawakuta ya Mubarrak wa Misri itakapofika mwaka 2014 pale Wazanzibari tutakapopitisha maamuzi yetu ya Muungano wa MKATABA.
 
Utamu wa KUTAWALA... KUNAIPONZA CCM na UONGOZI wake... Kwanza waiache ZANZIBAR iwe YENYEWE... ni KIDONDA NDUGU!!!
 
nawaunga mkono wazanzibari haiwezekani rais wa zanzibar akachaguliwa dodoma, hawa watu wana hoja ni vema ikajadiliwa kwa upana, NEC na CC ya CCM dodoma isiwaamulie wazanzibari nini wanataka, dr. bilali ni muhanga wa jambo hili pindi karume anapitishwa kuwa rais naamini watapigania haki yao.
 
Sasa wazanzibar wanataka NEC ya Zbar ndio ichague mgombea wao na jina ndio lipelekwe Dodoma kujadiliwa au kupitishwa?
 
Back
Top Bottom