Ahmed Ally: Tukichukua Ubingwa bado mtalaumu?

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
"Kwenye Boxing(masumbwi) kuna mashabiki bondia asiposhinda kwa knock out hawaridhiki, wanataka bondia ashinde sio kwa point bali kwa knock out. Ndivyo ilivyo hata kwenye soka, mashabiki wa Simba wanaolaumu timu kutovutia kiuchezaji wanapaswa kufahamu sisi msimu huu tunahitaji zaidi points"

"Msimu uliopita tuliongoza kwa kufunga mabao mengi kwenye ligi kuu Tanzania bara kuliko timu yoyote lakini hatukuwa mabingwa, sasa msimu huu tunataka kushinda mechi zote ikiwezekana bila kujali tumefunga mabao mangapi maana lengo ni Ubingwa tu na sio kitu kingine"

"Hao wanaotaka magoli mengi na mpira mzuri niwaulize, vipi kama tukishinda mechi zote na tukawa mabingwa watalaumu ?!"

"Hao waliofunga tano tano upepo umekata mbona wameanza kufunga mojamoja".
 
Aliye karibu na Ahmed Ally, viongozi Simba na benchi zima la ufundi la Simba awakumbushe kuwa inaweza kutokea mwishoni mwa ligi pointi zikalingana na bingwa akaamuliwa kutokana na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Tatizo la Simba kwa takribani miaka mitatu sasa wamekuwa na tabia ya kuridhika sana wakishafunga magoli mawili/matatu hivi basi biashara imeisha hata kama wanaweza kumfunga mtu kumi bila. Simba wakishafunga goli mbili/tatu basi utaona wachezaji umakini unapungua, wachezaji wanaanza kutembea na mpira uwanjani, mbwembwe hata mahali posipostahili, badala ya mpira kupelekwa mbele wanaanza kupiga pasi za kurudi nyuma, wachezaji kupigiana pasi fupi fupi wakiwa sehemu moja mpaka adui asogee, wanapooza mchezo kabisa, wakati mwingine washambuliaji wanasubiri mpira hata zaidi ya dakika kumi haufiki mbele, n.k. Yote hayo yanafanyika na benchi la ufundi lipo na wanakaa wanaangali wanaona ni sawa tu.

Imefika mahali sasa ukiangalia mechi ya Simba ukiona anaongoza goli mbili na timu ni kibonde hata kama ni dakika ya 30 kipindi cha kwanza ni bora uondoke ukafanye kazi zako nyingine vinginevyo utakuwa "bored" tu.

Ni mtizamo tu.
 
Haka kajamaa ni mtu aliyejulia mpira ukubwani, toka enzi utamaduni wa Simba ni kucheza mpira wa kuvutia, pira biriani lilianzia kwa SIMBA. Pamoja na matokeo mazuri bado Aina ya mpira wanaocheza hauvutii.
 
Mbona kuna takwimu zinazagaa mitandaoni kuwa Simba ndio timu iliyopiga pasi nyingi sana msimu huu kuliko timu zote Tanzania. Sasa unataka biriani gani tena wakati takwimu inaonesha kuwa ndio timu inayopasiana haswa? Dr Restart
 
Pasi nyingi si kigezo kucheza vizur
 
Kwahyo magoli manne ni MACHACHE….???
Mbona hayo yanapatikana mechi moja tu kati ya mechi 27 zilizosalia? Mtu akipigwa 7-0, si tayari hapo? Mbona hizi sherehe za magoli mengi zimeanza mapema sana wakati ligi ndo kwanza ipo mzunguko wa tatu?
 
1695936628157.png
 
Ndo usubiri yapatikane sasa boss…!! Ila kumbuka WEWE UPATE halafu uombee MWENZAKO AKOSE…!!!
 
Back
Top Bottom