Kama unajiuliza, unashangaa na kusikitika kwanini Simba SC inakamiwa, Wachezaji wake Kuumizwa vibaya na Ahadi nyingi Kutolewa haya ndiyo Majibu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
1. Yanga SC wameamua kuwa kwa Msimu huu iwe Mvua au Jua na kwa Mikakati yoyote ya ndani na nje ya Uwanja wanashinda.

2. Kuumiza kwa Makusudi Wachezaji wa Simba SC ili Timu itetereke na ikose muelekeo katika Ligi.

3. Baada ya Yanga SC Kutolewa Alfajiri tu huko CAF CL huku wakiwa hawataki Kuchekwa na Simba SC ambayo Kufika mbali ni Jadi yake Mkakati wa sasa ni Kuidhoofisha Kiuchezaji kwa Kuumiza Wachezaji Muhimu na itolewe mapema.

4. Mpango (Mkakati) uliopo ni Simba SC kupoteza Michezo ( Mechi ) zake Tano tu huku mwanzoni ili Wao Yanga SC watumie huo mwanya wa Kuihujumu Simba SC kupitia Kuhonga Timu Pinzani na Waamuzi (Referees) ambao mpaka sasa 85% yao wapo katika Payroll ya GSM.

5. Kuna Kontena kama Mbili au Tatu za Jezi zipo njiani hivyo ili Kuziuza vyema na GSM Kujipatia Faida Kubwa Mkakati ni kuhakikisha Yanga SC inashinda kwa Gharama yoyote ile huku ikiihujumu Simba SC ili kuleta mwamko na Hamasa Kubwa kwa Mashabiki wa Yanga SC na hatimaye Waaminishwe kuhusu Ubingwa wa mapema na waanza Kugombani Jezi Madukani.

6. GSM ambaye pia ndiyo Msimamizi wa Mchakato mzima wa Mabadiliko ya Yanga SC kuwa chini ya Wawekezaji anaanza Kujiandalia Mazingira ya Kuaminiwa na Kukabidhiwa sehemu kubwa ya Klabu ( Timu ) amepanga kutumia Pesa Kubwa ya Kuhonga, Kufanya Ushawishi na Kuimaliza Simba SC Kimchezo na hatimaye Yanga SC iwe Mikononi mwake ( mwao ) Kikatiba.

7. Uwoga mkubwa wa Viongozi wa Yanga SC na Mdhamini wao Mwandamizi GSM kwa Ahadi waliyoitoa mara ya Pili kuwa kwa Msimu huu wa 2021 / 2022 wamesajili Majembe na watakuwa Mabingwa isipotimia yanaweza kuwakuta makubwa kutoka kwa Mashabiki wa Yanga SC hivyo wanachokifanya sasa ni kutumia Pesa zaidi ya ile anayepata Bingwa wa Ligi Kuu Tsh Milioni 500 ili wawe Mabingwa na wawanyamazishe Mashabiki zao ambao Kiasili ni Wakorofi na hawana Uvumilivu pia.

Nuksi tumeshaitoa leo sasa mtatukoma.
 
Manara kawaingiza mkenge, alivyo sema kwenye interview kua anajua mbinu walizotumia simba kuhakikisha wanashinda mechi.

Viongozi wa yanga wakakurupuka na kurubunika kirahisi kua sababu ni kuhonga na fitna za kuwahonga timu pinzani kuhakikisha wanacheza rough

Wamesahau mafanikio ya simba hayakua tu ligi kuu bali hadi club bingwa huko simba ilikua na muendelezo mzuri, iliwezekana vipi simba kuhonga timu kama al ahly ili ipate matokeo. GSM kwa ubongo wake wa bundi ameshindwa kujiongeza
 
Siku zote Mda ni mwalimu mzuri Sana Ila Mpira unachezwa hadharani anayejua anajua Tu na Simba SC ni timu kubwa Nina Imani kama unenayo Yana chembe za ukweli Simba SC hatutokaa kimya ndo maana Halisi ya Nguvu moja
 
Mwanzo wa yanga hua ni ngumu kutabirika ila mwisho unajulikana

Mwaka jana yanga aliongoza ligi kwa kipindi kirefu tena akiwa unbeaten, mashabiki wakatamba sana japo ushindi wao ulikua ni wa penalty lakini uliwaridhisha.

Saizi wameshinda kimechi kimoja tayari wanajiona kama wamechukua ubingwa, wamesahau mwaka jana walishinda mechi zaidi ya moja na wakaongoza ligi na kombe likaenda msimbazi
 
Mkuu uko sahihi hili kila mwanamichezo tz analijua unganisha na hii picha ya Oscar oscar
Screenshot_20211001-155356.jpg
 
Kikao cha mambumbumbu, kwa timu gani hadi ihujumiwe time fwd mugalu mushimba
Hiyo hiyo ilochukua ubingwa wa nchi mara 4 mfululizo na kufika robo fainal caf championins ligi mara 2 mpka inaogopwa na alahly, kaizer, mamelodi na tumu zingine kubwa kubwa Africa mpka wanakuja kununua wachezaji wetu bora huku wewe ukitolewa mapema kabisaa hadi aibu kwa nchi na litimu letu la hovyo
 
Hiyo hiyo ilochukua ubingwa wa nchi mara 4 mfululizo na kufika robo fainal caf championins ligi mara 2 mpka inaogopwa na alahly, kaizer, mamelodi na tumu zingine kubwa kubwa Africa mpka wanakuja kununua wachezaji wetu bora huku wewe ukitolewa mapema kabisaa hadi aibu kwa nchi na litimu letu la hovyo
Ikaogopwa na nani? Umelogwa wewe kaizer kakuzabua kama mtoto 4, al ahly kachukua ubingwa afrika wewe wajisifia kufika robo kweli nyau fc wewe

Kununua wachezaji kwani kisinda ajanunuliwa huna timu ya maana mkuu
 
Back
Top Bottom