Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,473
- 757
YANGA ambayo iliwasili Cairo Alhamisi na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa maofisa wa ubalozi na Watanzania waishio nchini humo inakabiliwa na kibarua kigumu leo usiku itakapoikabili, Al Ahly, mabingwa watetezi wa Afrika katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa.
Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika michuano ya klabu Afrika ambao wamefadhiliwa na ubalozi wa Tanzania mjini Cairo kwa chakula na huduma nyingine muhimu wanaingia uwanjani wakiwa na dhamira ya kufuta uteja na rekodi mbaya dhidi ya Waarabu.
Al Ahly imeanza moja kwa moja raundi ya kwanza kutokana na kuwa ni bingwa mtetezi. Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Cairo.
Hata hivyo, timu hiyo iliyoiondoa Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro kwa mabao 14-1 na inayoundwa na wachezaji wengi wa Taifa Stars iliyokuwa ikishiriki michuano ya Afrika nchini Ivory Coast mwezi huu, wachezaji na viongozi wao wameahidi kupigana kufa au kupona ili kubadili historia ya soka Afrika.
Nyota wake, Mkenya, Boniface Ambani aliyekuwa China kwa majaribio ya soka la kulipwa ataisaidiwa katika mchezo huo na Mrisho Ngassa, Ben Mwalala, Jerson Tegete na Mike Barasa katika ushambuliaji wakisaka mabao, ingawa wana kibarua kigumu cha kuwapita mabeki na ukuta mgumu wa Ahly.
Pia, kwa upande wa ulinzi, Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub 'Cannavaro', Nurdin Bakari wana jukumu zito la kumlinda kipa Juma Kaseja au Mserbia Obren Curkovic, ambao mmoja kati yao ndiye atayekuwa katikati ya milingoti mitatu.
Katika kiungo wanatarajiwa Godfrey Bonny, Athuman Idd 'Chuji', wachezaji wa Stars ambao waliondoka wakiahidi kucheza kwa bidii na maarifa ili kulinda heshima ya nchi yao.
Tangu kuwasili Cairo, baadhi ya wachezaji wa Yanga, akiwamo Mrisho Ngassa wamekuwa gumzo, wakifuatiliwa pia na vyombo vya habari vya hapa ambavyo vinaisifu timu yao, huku kocha Dusan Kondic akiwajibu wanahabari kuwa wasubiri kuiona uwanjani timu yake ambayo imejiandaa vizuri kwa mchezo huo.
Kondic ameahidi kuwa vijana wake watacheza kwa bidii na maarifa kama alivyowaelekeza ili kuiondoa Ahly katika michuano ya Afrika mwaka huu
braza mm nipo Misri hapa lakini si cairo, nipo mji mbali kidogo wa Alexandria, niseme ukweli nawafahamu Ahly na hawa jamaa wanawashabiki wengi sana kuliko timu yoyote hapa Misri, uwezo wanao kweli japo marefa huwabeba wakti fulani, Yanga wana mlima wa kupanda japo mpira unadunda.Wana JF na wapenzi wa soka Tanzania na kwingineko duniani kesho ile mechi ya Yanga na El Ahly au National Athletic Club ya Egypt ndio itakuwa inapigwa mida ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika mashariki. Kwa mlioko Misri au wenye uwezo wa kuona mechi hii live muwe mnatuupdate hapo kesho mechi itakapoaanza.
Je wajua;
Mechi itapigwa kwenye dimba la Cairo international Stadium lenye uwezo wa kuchukua watu 74,100. Uwanja huo upo katika kitongoji cha Nasr ndani ya jiji la Cairo na ulifunguliwa mwaka 1960.
Mafanikio yao katika mashindano mbali mbali ni kama ifuatavyo;
Egyptian League (31) (Egyptian Record): 1948/49, 1949/50, 1950/51, 1952/53, 1953/54, 1955/56, 1956/57, 1957/58 , 1958/59, 1960/61, 1961/62, 1974/75, 1975/76, 1976/77, 1978/79, 1979/80, 1980/81, 1981/82, 1984/85, 1985/86, 1986/87, 1988/89, 1993/94, 1994/95, 1995/96, 1996/97, 1997/98, 1998/99, 1999/00, 2004/05, 2005/06
Egyptian Soccer Cup (34) (Egyptian Record): 1923/24, 1924/25, 1926/27, 1927/28, 1929/30, 1930/31, 1936/37, 1939/40, 1941/42, 1942/43, 1944/45, 1945/46, 1946/47, 1948/49, 1949/50, 1950/51, 1952/53, 1955/56, 1957/58, 1960/61, 1965/66, 1977/78, 1980/81, 1982/83, 1983/84, 1984/85, 1988/89, 1990/91, 1991/92, 1992/93, 1995/96, 2000/01, 2002/03, 2005/06
Egyptian Super Cup (3) (Egyptian Record): 2003, 2005, 2006
Sultan Hussein Cup (7): 1922/23, 1923/24, 1925/26, 1926/27, 1928/29, 1930/31, 1938/39
Cairo League (5): 1938/39, 1941/42, 1942/43, 1947/48, 1949/50
United Arab Republic League (1): 1960/61
African Championships
CAF Champions League (5) (Current Champion, African Record): 1982, 1987, 2001, 2005, 2006
African Cup Winner's Cup (4) (African Record): 1984,1985,1986, 1993
CAF Super Cup (2) (Current Champion, African Record):2002, 2006, 2007
Medalla de bronce en Japón:2006
Afro-Asian Cup (1):1989
Century Cup (Al-Ahly vs. Real Madrid) (1): 2001
Arab Champions Cup (1): 1996
Arab Cup Winners Cup (1):: 1995
Arab Super Cup (2): 1997, 1998
Kocha wao ni Manuel José de Jesus ambaye ni raia wa URENO, timu kapteni niEmad Meteeb na raisi wa club ni Hassan Hamdy mbaye yupo madarakani toka Mei 2002.
Timu yao ya sasa ina wachezaji wafuatao;
1
POR
Essam El-Hadary
2
DEF
Islam El-Shater
4
DEF
Emad El-Nahhas
5
DEF
Ahmad El-Sayed
6
DEF
Ahmad Sedik
7
DEF
Shady Mohamed (capitán)
8
MED
Mohamed Barakat
9
DEL
Emad Moteab
10
DEL
Ahmed Belal
11
MED
Tarek El-Saiid
12
DEF
Sebastiao Gilberto
14
MED
Hassan Mostafa
15
DEF
Abdulilah Galal
17
MED
Anis Boujelbene
18
DEL
Osama Hosny
No.
Posición
Jugador
19
DEL
Akwety Mensah
20
MED
Mohamed Shawky
21
MED
Mohamed Abdullah
22
MED
Mohamed Aboutrika
23
DEL
Flávio Amado
24
MED
Ahmad Hassan Stakoza
25
MED
Hossam Ashour
26
DEF
Wael Gomaa
27
POR
Amir AbdulHamid
28
POR
Nader El-Sayed
29
DEF
Ahmad Shedid Qinawi
30
DEF
Mohamed Sedik
31
DEF
Ahmed Adel
32
MED
Haitham Al Fazani
33
DEL
AbdelHameed Hassan
Haya wanajangwani na watanzania kwa ujumla kesho kazi tunayo na tunaomba Mungu tuweze kuwaangusha vinara hawa wa soka Afrika na kuweka historia mpya ya soka Tanzania na Afrika.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
kama itokea yanga akapata matokeo hayo basi uwezekano wa kusonga mbele upo.....ila mimi ningependa apigwe kama 3-0 au zaidi, maana sipendi kuwa mnafiki siwa pendi yanga kama manu vile...halafu hapa ningependa apate ushindi wa 2-1 au sare yaani hapo nitakuwa nimefurahi kweli kweli....lkn watani yanga mwaka huu ana kikosi kizuri kuliko miaka yote niliyopata kuiona yanga...naomba mfungweMimi natabiri mechi itaisha kwa sie Yanga kushinda 2-1