Ahadi kila kijiji kupata milioni 50/- sasa yaiva, Serikali yatenga jumla ya Sh bilioni 811

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
SERIKALI imetenga jumla ya Sh bilioni 811 zitakazotumika kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kukipatia kila kijiji Sh milioni 50 kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Imeelezwa kwamba serikali imeshaanza kushirikisha wadau mbalimbali kupata maoni ya jinsi ya kuendesha mpango huo kwa ufanisi na tija.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) alisema serikali itaanza kutoa fedha hizo kuanzia mwaka wa fedha ujao. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya mkutano wa wadau waliokuwa wanajadili rasimu ya mpango huo wa utoaji fedha kwa ajili ya maendeleo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa halmashauri za wilaya, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), mabenki, mifuko ya hifadhi ya jamii na vikundi mbalimbali. “Kwa kuanzia, fedha hizo zitatolewa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka mitano,” alisema.

Alisema fedha hizo zitatolewa kupitia benki kabla ya kutolewa kwa vikundi mbalimbali kama Vicoba, Saccos na vikundi vingine kulingana na taratibu zitakazowekwa. Alisema mpango utaanza na mikoa 10 iliyo nyuma katika kutumia huduma za kifedha kwa kuzingatia taarifa ya utafiti ya Finscope ya mwaka 2013.

Mikoa hiyo ni Singida, Lindi, Mtwara, Mbeya, Shinyanga, Geita, Kagera, Dodoma, Rukwa na Ruvuma. Akifungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uhusiano ya Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, alisema mkutano huo ulilenga kupata maoni ya wataalamu ya namna bora ya kuutekeleza.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri, Kaimu Mkurugenzi, Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Victor Mwainyekule alisema mawazo yaliyopatikana yatazingatiwa kuboresha mpango huo unaolenga kupambana na umaskini.

Mkuu wa Uendeshaji, Benki ya Wanawake (TwB), Zablon Yebete alisema mpango huo ni uwekezaji mkubwa kwa Watanzania unaopaswa kuungwa mkono na vyombo vya fedha na wadau wengine nchini.

“Tunatakiwa kuunga mkono mpango huu unaohusisha vyombo vya fedha katika utekelezaji wake kwa faida ya taifa,” alisema. Kwa mujibu wa mpango huo, walengwa watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kupatiwa fedha hizo.
Chanzo: Habarileo
 
Serikali lazima iwe careful kwenye hii program isije ikawa kama kwenye ‘’mabilioni ya Rais Kikwete’’ ambapo zaidi ya Sh bilioni 43.69 zilitolewa ili kunufaisha wajasiriamali lakini ikaishia kuwa whitewash!

Ninaamini kuna baadhi ya watu ambao sio walengwa lakini wanasubiri kwa shauku kubwa kunufaika bila kujali kama watatumbuliwa au la.

Mmarekani Williams aliwahi kusema, ‘’A smart man makes a mistake, learns from it, and never makes that mistake again. But a wise man finds a smart man and learns from him how to avoid the mistake altogether’’.

Hopefully, our government is smart enough and wise enough.
 
Walipaswa wawe wameanza kutoa Trainiing kwa Viongozi wa Serikali za vijiji kuhusu management ya hizo pesa

Waweke mikakati ya kupima matokeo ya uwekezaji wa fedha hizo na mrejesho.Vinginevyo ni yaleyale ya JK.
 
Hawajasema specific time watakapoanza kuzitoa hizo pesa lakini ninadhani muda siyo rafiki yao.

Mwaka ujao wa fedha uko around the corner wakati kwa sasa wadau bado wanapitia rasimu na kutoa maoni zaidi ili kuiboresha. Ninadhani watachelewa sana kuanza hili zoezi.
 
Walipaswa wawe wameanza kutoa Trainiing kwa Viongozi wa Serikali za vijiji kuhusu management ya hizo pesa

Waweke mikakati ya kupima matokeo ya uwekezaji wa fedha hizo na mrejesho.Vinginevyo ni yaleyale ya JK.

Nakubaliana na wewe kabisa hapo! Wasifanye haraka waandae mazingira kwanza lkn nina Imani na Waziri Mpango kwamba ni mtu makini sana!
 
SERIKALI imetenga jumla ya Sh bilioni 811 zitakazotumika kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kukipatia kila kijiji Sh milioni 50 kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Imeelezwa kwamba serikali imeshaanza kushirikisha wadau mbalimbali kupata maoni ya jinsi ya kuendesha mpango huo kwa ufanisi na tija.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) alisema serikali itaanza kutoa fedha hizo kuanzia mwaka wa fedha ujao. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya mkutano wa wadau waliokuwa wanajadili rasimu ya mpango huo wa utoaji fedha kwa ajili ya maendeleo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa halmashauri za wilaya, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), mabenki, mifuko ya hifadhi ya jamii na vikundi mbalimbali. “Kwa kuanzia, fedha hizo zitatolewa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka mitano,” alisema.

Alisema fedha hizo zitatolewa kupitia benki kabla ya kutolewa kwa vikundi mbalimbali kama Vicoba, Saccos na vikundi vingine kulingana na taratibu zitakazowekwa. Alisema mpango utaanza na mikoa 10 iliyo nyuma katika kutumia huduma za kifedha kwa kuzingatia taarifa ya utafiti ya Finscope ya mwaka 2013.

Mikoa hiyo ni Singida, Lindi, Mtwara, Mbeya, Shinyanga, Geita, Kagera, Dodoma, Rukwa na Ruvuma. Akifungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uhusiano ya Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, alisema mkutano huo ulilenga kupata maoni ya wataalamu ya namna bora ya kuutekeleza.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri, Kaimu Mkurugenzi, Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Victor Mwainyekule alisema mawazo yaliyopatikana yatazingatiwa kuboresha mpango huo unaolenga kupambana na umaskini.

Mkuu wa Uendeshaji, Benki ya Wanawake (TwB), Zablon Yebete alisema mpango huo ni uwekezaji mkubwa kwa Watanzania unaopaswa kuungwa mkono na vyombo vya fedha na wadau wengine nchini.

“Tunatakiwa kuunga mkono mpango huu unaohusisha vyombo vya fedha katika utekelezaji wake kwa faida ya taifa,” alisema. Kwa mujibu wa mpango huo, walengwa watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kupatiwa fedha hizo.
Chanzo: Habarileo
Msingi ni kuangalia njia sahihi za kutoa hizo pesa na vilevile jinsi ya kuzifanyia monitoring baada ya kutumika ili kuona matokeo yake na pia ni vizuri watendaji wa Kijiji wakawa equiped na maarifa pia hasa wale ambao hawana maarifa, vijiji ambayo vina miradi tayari inayofanana na hiyo ni vizuri wangeanza kuviintagrate ili kupunguza gharama za mafunzo
 
Wazo ni zuri sana japo kwenye selection ya mikoa inayoanza ndio inanipa ukakasi. Nashauri ianzie mikoa yenye kipata duni zaidi. Najaribu kuwaza jinsi geographically KAgera ilivyo ndogo kwenli ukilinganisha na mkoa kama Tabora kweli?!?!?!? Nashauri wachukue mikoa kumi iliyo na kipato cha chini kuliko yote ndio ianzie Huko. Jenista Mhagama are you sure huna Conflict of Interest hapo?????!!!
 
Back
Top Bottom