Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,202
- 138,568
Kamati ya Ukweli na Maridhiano ya Chama cha Tanzania Labour (TLP), imetangaza kumvua uanachama Mwenyekiti wa chama hicho, Agustino Mrema.
Akizungumza jana, jijini Dar es Salaam na MTANZANIA Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joram Kinanda alisema kuwa kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia kwa kina malalamiko yaliyokuwa yakimuhusu Mrema, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mbali na Mrema wengine waliovuliwa uanachama ni Hamisi Mkadamu, Antoni Mapunda, Nancy Mrikaria, Dominata Rwechungura, Maxmilian Lymo, Richad Lyimo, Hamisi Mkumba na Stanley Temba.
Kinanda alisema kuwa wanachama hao wamevuliwa uanachama kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, toleo la 2005 Ibara ya 9.9 (c) na 2009 ibara 9.5(c).
Kinanda alisema kuwa maazimio hayo yamepelekwa katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa taratibu za kisheria pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza, alipotafutwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema kamati hiyo haitambuliki kisheria.
"Kamati hiyo haitambuliki kisheria, na hata Mrema mwenyewe amekuwa akipinga TLP kuwa na kamati ya aina hiyo na hata viongozi wake hawatambuliki, " alisema
Ni sawa na Chadema imvue uanachama Mbowe kwa kukibadilisha kinyemela kifungu cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya chama. Ni kitu kisichowezekana.
Ni sawa na Chadema imvue uanachama Mbowe kwa kukibadilisha kinyemela kifungu cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya chama. Ni kitu kisichowezekana.
Mtanzania, Tanzania Daima hayaaminiki sana, tungoje uthibitisho mwingine,, hata hivyo Mrema siasa imeshamchoka kitambo!
Mrema ni mmiliki wa chama kama alivyo Mbowe, hawezi kufukuzwa.

Vyama vya upinzani ni sawa na comedy.
CHADEMA ni mali ya MBOWE na ukoo wa ndesa, hata kabla ya uchaguzi mkuu , familia imeshateua wabunge wa viti maalumu toka kwenye ukoo, piga wale ndugu, wake na wenye ukoo na wenye kuimiliki CHADEMA lazima watakuwa wabunge wa viti maalumu chadema mwaka huu baada ya uchaguzi
Usanii wa ccm mpaka leo hamjampa mafao yake ya cheo feki cha unaibu uwaziri mkuu.ccm kibokoMrema ni mmiliki wa chama kama alivyo Mbowe, hawezi kufukuzwa.