Agongwa wakati akitoroka matibabu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KIJANA Musa anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-25, amegongwa na gari wakati akitoroka matibatu katika hospitali ya Temeke ya jijini Dar es Salaam.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Faustine Shilogile, alisema jana kuwa, Musa aligomngwa na gari mara baada ya kutoroka hospitalini alipokuwa anatibiwa.

Alisema marehemu huyo ambaye alikuwa akisumbuliwa na malaria kali alikuwa akitibiwa hospitalini hapo na aligongwa na gari jana alfajiri katika Barabara ya Sokoine wakati akitoroka matibabu.

Alisema mashuhuda walimuona Musa akitoka hospitalini hapo huku akikimbia na baadae wakapata taarifa kuwa amegonjwa katika barabar hiyo majiara hayo ya alfajiri.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini, na polisi wanaendelea kumtafuta dereva aliyesababisha kifo hicho.

Katika tukio jingine mtu mmoja amefariki na mwingine kujeruhiwa wakati walipogongwa na gari aina ya Fuso wakiwa wanatumia usafiri wa pikipki.

Watu hao waligongwa jana majira ya jioni, katika barabara ya Kawawa.

Mwili huo ulichukuliwa na kwenea kuhifadhiwa hosptitali ya Temeke.
 
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.
Huenda tayari malaria ilikuwa imesha panda kichwani.
Lakini Waswahili utawasikia wakisema eti ni mkono wa mtu.
 
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.
Huenda tayari malaria ilikuwa imesha panda kichwani.
Lakini Waswahili utawasikia wakisema eti ni mkono wa mtu.

Hapo juu kama ulikuwepo... Hata sijui lini tutajifunza ku-face reality
We always seem to look for an escape route
 
Duh! pole sana

Usiombe Malaria kupanda kichwani; iliwahi kunitokea vituko nilivyofanya ndani ya wiki 1 mmoja huwa vinasimuliwa mpaka leo! na yapata miaka 18 sasa !Nawashukuru watu wa karibu yangu walihakikisha napata tiba!

Inasikitisha sana na siajabu alijipeleka mwenyewe hospitali na alikosa mtu wa kumsimamia matibabu.
 
Halafu viongozi wetu wanapigia debe Net badala ya kuangamiza vimelea vya Mbu! RIP Musa. Malaria hai.....
 
Back
Top Bottom