Agizo la Mhe Rais laendelea kutekelezwa Samanjiro..

Agizo la Mhe Rais laendelea kutekelezwa Samanjiro..

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Agizo la Rais Dr. John Pombe Magufuli, kuwa wafanya biashara wadogo (machinga) wapewe vitambulisho vya biashara linaendelea kutekelezwa, wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Kaimu mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mhandisi Tumaini Magesa akizungumza na wafanya biashara hao leo tar 5.01.3019 amesema Rais ana nia njema kwa wananchi wake.

"Iko njia njema ya Rais Dr.John Pombe Magufuli kuwatambua na kuwarasimisha wafanya biashara wadogo kwa kuwatambua na kuwapa vitambulisho.."

Alisema hakuna nchi Duniani iliyoendelea bila kodi, ambapo aliwataka wananchi hao kutokwepa kulipa kodi kuwa hizo ndizo zinazoendesha nchi.

Akizungumza mbele ya wafanya biashara hao, Zuwena Omary Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro alisema, hakuna faini kwa atakayefika TRA kulipa kama hakuwa kwenye mfumo wa ulipaji kodi kama machinga.

Alisema elimu ya mlipa kodi itaendelea kutolewa sambamba na zoezi la ugawaji vitambulisho hivyo kwa siku saba, hivyo fursa bado ipo.

Alisema kwa waliopata vitambulisho hivyo watahakikiwa tena na TRA na kama wataonekana kuwa hawana sifa kama machinga watatakiwa kulipa kodi TRA kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi walisema wengi wao walihamasika kwenda TRA kuchukua TIN namba kwa lengo la kupata mikopo tofauti na maelekezo ya sasa.

"Wengi wetu hatuna mitaji ya kiwango cha kulipa kodi TRA naomba Serikali itusaidie kwani bado hali sio nzuri kiuchumi" walisema baadhi ya wananchi.

Akijumuisha hoja hizo, Yefred Myenzi mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro alisema, watu wengi hawako tayari na hawapendi kulipa kodi.

Alisema wakati mwingine maafisa wa TRA wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kwa wafanya biashara kudai kodi, na kuwataka wawe na utamaduni wa kulipa kodi.

Zoezi la ugawaji vitambulisho wilayani Simanjiro limezinduliwa leo tar 5.01. 2019 na litaendelea sambamba na kutolewa elimu kwa wafanya biashara kama lilivyo kusudio la Rais Dr. John Pombe Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • IMG-20190105-WA0171.jpg
    IMG-20190105-WA0171.jpg
    90.9 KB · Views: 22
  • IMG-20190105-WA0172.jpg
    IMG-20190105-WA0172.jpg
    80.2 KB · Views: 23
Back
Top Bottom