Agenda za M4C - USHAURI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Agenda za M4C - USHAURI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbogela, May 29, 2012.

 1. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa Kila Mtanzania mpenda mabadiriko na Mtanzania yeyote anayetaka kuona nchi hii ikienda kwenye mstari wa Neema hataacha kufuatilia M4C aka Vua Gamba Vaa Gwanda. Katika Mikutano yote ya M4C tumeona umati mkubwa sana ukimiminika. Na kama ambavyo kila mtu anajua kuwa walipo wengi pana Mengi naamini pia interest za wasikilizaji nazo zinatofautiana kwenye mada wanazotaka kusikia.Uongozi wa CHADEMA umefanya jambo zuri sana kuhakikisha kuwa kuna wasemaji mbali mbali katika mikutano hiyo. Lakini nadhani wasemaji wakuu wamekuwa na hoja zinazofanana fanana. Mathalani mkutano wa DAR hoja ya KATIBA ilichukua sehemu kubwa. Hivyo basi ushauri wangu wa Kwanza ningependa wasemaji wakuu wa M4C wangegawana maeneo ya kuwakilisha, mwingine awakilishe hali ya Uchumi na Maisha ya watanzania, Mwingine awakilishe Sheria na haki za Raia, Mwingine Awakilishe Huduma za Jamii (Afya, Elimu, Maji, Umeme nk), Hoja ya UFISADI isiachwe nadhani ni HOJA muhimu wasiogope madongo ya CCM kuwa CHADEMA hawana Hoja wana hoja ya UFISADI tu, nadhani mifano ya hivi karibuni itumike kuchambua UFISADI ulivyoota mizizi na kuwa hauwezi kuachwa au kuondoka ndani ya serikali ya CCM na kuunganisha UFISADI na unavyosababisha umasikini miongoni mwa jamii ya watanzania na matokeo yake ndio MAISHA MAGUMU kwa KILA mwana wa NCHI.Hata hivyo ninadhani kuna AJENDA moja muhimu sana imeachwa, AJENDA ya inayoeleza nguvu na siraha waliyonayo wananchi katika kubadiri serikali siraha ya KURA. Mimi naamini kuwa mpaka 2015 vijana wataendelea kuwa nguzo ya ushindi wa CHADEMA. Vijana wengi ni pamoja na wale ambao hawajawahi kupiga kura kabisa. Vijana waliozaliwa baada ya 1992 watahitaji kupiga kura kwa mara ya kwanza 2015. Hivi karibuni Tume ya Uchaguzi itaboresha daftari la kudumu la wapiga kura. Na inakadiriwa zaidi ya wapiga kura milioni 6 wapya wataandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa vijana tunategemea waingie katika daftari hilo. Sasa basi huu ni muda Muafaka kwa CHADEMA kupitia M4C kuhamasisha vijana wajiandae kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. AJENDA ya KUJIANDIKISHA, KUTUNZA KADI na kisha Kushiriki katika KUPIGA KURA wakati muafaka ukifika iongelewe kwa msisitizo. Ushauri wangu wa PILI ndio huo kuwa kwenye M4C CDM waongeze msisitizo kwenye AJENDA inyohusiana na kujiandikisha. Mpaka sasa M4C a.k.a VUA GaMBa Vaa GWaNDa Imefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana, lakini nadhani nikiwa kama mtanzania mwenye uchungu na nchi hii na mwenye nia ya kuona kuna mabadiriko Chanya katika nchi yetu basi ningependa kutoa mawazo na ushauri kuweza kuboresha zaidi vugu vugu la mageuzi.Nawakilisha
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Wamekusikia mfano..lema azungumzie ugumu wa maisha
   
Loading...