Big Phil
Member
- Nov 20, 2019
- 50
- 338
Habari!
Kumekuwa na taarifa nyingi za kushtusha za mauaji ya wanandoa, watoto, na kesi nyingi Sana za kushtusha ambazo mwanzoni hazikuwa zinatokea mara kwa mara kama ilivyo sasa hivi. Huwa na jiuliza tatizo ni nini haswa.
1. Maisha magumu?
2. Mmong'onyoko wa maadili kwenye jamii zetu.
3. Stress
Nakuja kugundua ni afya ya akili. Wengi wetu kwenye jamii tunasumbuliwa na tatizo la afya ya akili (Mental health) bila kujua na tatizo la afya ya akili halipewi nafasi kubwa kwenye jamii yetu na kufanya watu wengi tuishi kwa mazoea. Mfano juzi kijana ambaye ana miezi 4 tu kwenye ndoa kamuua mke wake kwa kumpiga bastola mara 7, na yeye kujiua kwa kujipiga bastola. Ili ni tukio la kuhuzunisha sana na kusikitisha pia, lakini kiini chake ni tatizo la akili. Wenzetu nchi zilizoendelea wana vitengo vya marriage counselling ambapo kunawapa nafasi wanandoa kujadili matatizo yao na kuyapatia suluhu na kama ikishindikana basi kupeana talaka, Zanzibar baba mzazi kumuingilia binti yake wa kumzaa kinyume na maumbile na matukio mengine maovu kwenye jamii. Nadhani ni wakati muafaka kwa nchi yetu kulitambua tatizo la afya ya akili na kulipatia ufumbuzi kuzuia mauji, ubakaji na kulinda jamii yetu ya Kitanzania.
Article inayokuja nitaelezea tatizo ya afya ya akili na namna gani unaweza kutibu.