Afya na magonjwa ya uzeeni

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari wanajf nipende kuwakaribisha katika uzi huu unaohusu afya hasa wakati wa uzeeni

1)Shida ya kutoona vizuri
Baada ya miaka 40 Watu wengi hupata ya kuona vizuri vitu vilivyo karibu na wanaweza kutibiwa kwa kupimwa na kuvaa miwani.

2)Udhaifu, Uchovu wa tabia za kula chakula
Inaeleweka Kuwa Watu wa makamo huwa hawana nguvu kama vile walipokuwa vijana na watazidi Kuwa dhaifu kama hawatokula chakula vizuri. Hivyo wanatakiwa wale vyakula vya kujenga na kukinga mwili japokuwa inaeleweka Kuwa hawali chakula cha kutosha.

3) Kuvimba miguu
Hii husababishwa na magonjwa ya aina nyingi lakini kwa upande wa wazee husababishwa na matatizo ya mzunguko wa damu pamoja na matatizo ya moyo. Tiba bora ya hivi ni kuinua juu na kupumzisha miguu. Usisimame wala kukaa huku miguu ikiwa chini(peku) weka miguu juu kila wakati.

4) Donda ndugu miguuni
Hutokanana na mzunguko mbaya wa damu hasa uvimbe wa neva mara nyingine husababishwa na ugonjwa wa kisukari.
Donda linalosababishwa na mzunguko mdogo wa damu huchelewa sana kupona.
Liweke donda ndugu katika hali ya usafi.

5) Kuziba mkojo
Wazee wa kiume walio na tatizo la kupata haja ndogo husababishwa na uvimbe katika kibofu cha mkojo au mawe katika figo au kibofu.

6) kikohozi cha muda mrefu
Kama mzee anakikohozi basi aache kuvuta sigara lakini pia wakati mwingine tatizo la moyo huenda likahusika.

7) Maumivu ya viungo
Kufanya mazoezi ndio suluhisho tosha kwa tatizo hili.

8) Matatizo ya moyo
Maoni kwa vijana kama wanataka kuishi maisha na afya nzuri uzeeni.
*kula vizuri
*Usiwe mlevi
*Usivute sigara
*Fanya mazoezi ya mwili
*Jaribu kupumzika na kulala usingizi wa kutosha
*Jifunze namna ya kutulia

AHSANTE
FB_IMG_16322406959039519.jpg
 
Back
Top Bottom