Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,638
- 22,490
Kuna wakati humu JF nilitoa ushauri kwa Prof Muhongo kwamba ili kuepukana na tatizo la umeme nchini, aache kabisa kuiingiza Tanzania kwenye mikataba midogo midogo ya uzalishaji umeme chini ya 300MW. Mikataba kama hiyo awaachie watu wa REA. Hata nilimwambia, ukiangalia Afrika Kusini, ni kama wangeweza kutupa umeme wa nchi nzima na ziada kwa kutumia mtambo wao mmoja tu!
Ushauri kwa Prof. Muhongo: Nguvu ya mradi wa Songas hailingani na kinachozalishwa, tusirudie kosa
Labda alinisikia. Sasa hivi Tanzania iko katika hatua za mwisho za makubaliano na kampuni kutoka Afrika Kusini, Kibo Mining, kuelekea kufunga mtambo wa umeme wa makaa ya mawe kule Mbeya wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa 250-350MW.
Mtambo huu wa umeme ukikamilika na kuanza kazi, utakuwa ni mtambo wenye kuzalisha umeme mkubwa kuliko yote iliyopo nchini, kutia na ile ya gesi tunayojivunia sana. Itamaanisha mtambo mmoja wa hii kampuni utakuwa unazalisha karibu 30% ya mahitaji ya umeme Tanzania.
Sasa swali ni kwamba, ikiwa kampuni hii inafunga mtambo mmoja tu na tunapata 30% ya umeme unaohitajika nchini, tumeshindwaje kutumia gesi yetu na kuwa na mitambo miwili tu ambayo itazalisha zaidi ya mahitaji yetu ya umeme? Kwa nini tunakuwa na gesi nyingi hivi, na bado tunaingia mikataba ya miradi midogo midogo ya kuzalisha umeme ya uwezo wa 100-150MW, ambayo inatuongezea gharama za mobilization bila sababu za msingi?
Source: African News Agency
Kibo Mining holds talks to accelerate development of Mbeya Coal to Power Project | IOL