Inanitatiza saana jinsi wamagharibi wanavyoiwinda Libya, na mara kadhaa wamekiuka azimio la UN juu ya kuwalinda raia na sasa wamepeleka na shehena za silaha kwa hao rebels na baraza lao ili kuimarisha mapigano na kuongeza idadi ya vifo ambavyo vingalizuilika. Kwa mstaarabu yeyote na mwenye chembe za kweli za huruma kwa binaadam wenzake...katu hawezi kuendelea kumwagilia petroli ili kuwepo na milipuko zaidi ya vifo, wahanga, walemavu watakaobadilika na kuwa tegemezi, uharibifu wa miundo mbinu etc.
Na hata hao waasi punde watakaa mezani tu ku-negotiate peace treaty na Ghaddafi, kwani mpaka leo hii miji ya Benghazi na Misrata tayari ipo katika uhaba mkubwa wa fedha na chakula. Ambapo raia hawatokubali kuridhia baa hilo la njaa kwa kisa cha kumuondoa madarakani Ghaddafi, si muda mrefu dunia itashuhudia aidha peace treaty au civil war na nchi ya Libya kugawanyika kabisa na kutotawalika abadan...ambapo ndio mwanzo wa kuumbuka kwa ukurupukaji wa kimaamuzi wa baraza la usalama la UN.
Pale Syria hali ni mbaya sana kwa wafuatiliaji wa purukushani za kumuondoa Bashar Al-Assad, ambapo ijumaa takriban watu milioni 1 waliandamana na fierce battles zilitokea na mauaji kufikia zaidi ya raia 1,000/= tangu maandamano nchini humo kuanza, lakini UN inaingia na inatoka na kutoa kemeo via microphones za press conferences lakini UN resolutions bado hazijachukulika. Kwa mwerevu haimpi taabu kubaini iwapo pale Syria au Somalia nchi za magharibi zitanufaikaje iwapo wakianzisha millitary missions za peace keeping kwa wananchi. Libya kuna asali taam na matunda yenye harufu ivutiayo.