Afrika kamwe Tusiwaamini Wakenya na ICC yao!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hivi karibuni tumesikia Viongozi wa Kenya wakizunguka Bara zima la Afrika kujaribu kulishawishi kujitoa ICC mpaka wakafanikiwa kufanya moja kati ya ajenda kubwa kwenye Mkutano wa viongozi wa Kiafrika huko Maua Mapya (Addis Ababa)!

Kama kuna jambo ambalo historia inaweza kutufundisha kitu nalo ni kwamba kamwe Afrika isiwaamini Wakenya na hapa namaanisha Viongozi maelite wa Kenya na siyo Mkenya mwananchi wa kawaida!

Maelite wa Kenya ni wabinafsi sana ni nani amesahau wakati wa Apartheid AK wakati Bara zima la Afrika lilipovunja Uhusiano na makaburu Kenya ilibakiza uhusiano na Makaburu, hata nchi za Waarabu kama Algeria zilisaidia sana nchi za Kiafrika klk Kenya, Wakenya (maelite) walikuwa wanakwenda hata kusoma AK, kwa kifupi Kenya kama nchi haikusadia kwa lolote kwenye mapambano dhidi ya Utawala wa Ubaguzi wa Waafrika wenzetu huko AK kwanza walikuwa upande wa Wazungu, nchi ya Kenya haina rekodi yoyote ile ya kujitoa kwa ajili ya kupigania Uhuru na heshima ya Mwafrika kama kuna mtu ana ushahidi ni wapi na lini nchi hiyo ilishiriki kusaidia Waafrika wenzetu popote pale auweke hapa usinitajie Somalia kwa maana Somalia wameambiwa na Wazungu waende huko na siyo wao wenyewe!

Sasa ni ajabu leo hii nchi ya Kenya kwa sababu Wazungu wao wamewageuka na sasa wanataka kuwaweka ndani Viongozi wao ICC wanataka Bara la Afrika liwakingie kifua, wakati Afrika inawahitaji walikuwa wako busy na Wazungu, hivyo naishauri nchi yangu ya TanZania ingawaje mimi siyo muumini wa hii ICC lkn nisingependa TanZania yangu iunge mkono jitihada za Kenya dhidi ya ICC, wacha Wazungu wawafundishe somo, na bado Wazungu wako na ninyi muda mrefu sana ujao mpaka mje kutambua kwamba Mzungu siyo rafiki wa Mwafrika bali ni adui, moto unakuja mwakani 2017 kwenye uchaguzi wenu, hapo ndiyo mtamjua Mzungu ile ya 2007 ilikuwa cha mtoto!
 
Hivi karibuni tumesikia Viongozi wa Kenya wakizunguka Bara zima la Afrika kujaribu kulishawishi kujitoa ICC mpaka wakafanikiwa kufanya moja kati ya ajenda kubwa kwenye Mkutano wa viongozi wa Kiafrika huko Maua Mapya (Addis Ababa)!

Kama kuna jambo ambalo historia inaweza kutufundisha kitu nalo ni kwamba kamwe Afrika isiwaamini Wakenya na hapa namaanisha Viongozi maelite wa Kenya na siyo Mkenya mwananchi wa kawaida!

Maelite wa Kenya ni wabinafsi sana ni nani amesahau wakati wa Apartheid AK wakati Bara zima la Afrika lilipovunja Uhusiano na makaburu Kenya ilibakiza uhusiano na Makaburu, hata nchi za Waarabu kama Algeria zilisaidia sana nchi za Kiafrika klk Kenya, Wakenya (maelite) walikuwa wanakwenda hata kusoma AK, kwa kifupi Kenya kama nchi haikusadia kwa lolote kwenye mapambano dhidi ya Utawala wa Ubaguzi wa Waafrika wenzetu huko AK kwanza walikuwa upande wa Wazungu, nchi ya Kenya haina rekodi yoyote ile ya kujitoa kwa ajili ya kupigania Uhuru na heshima ya Mwafrika kama kuna mtu ana ushahidi ni wapi na lini nchi hiyo ilishiriki kusaidia Waarika wenzetu popote pale auweke hapa usinitajie Somalia kwa maana Somalia wameambiwa na Wazungu waende huko na siyo wao wenyewe!

Sasa ni ajabu leo hii nchi ya Kenya kwa sababu Wazungu wao wamewageuka na sasa wanataka kuwaweka ndani Viongozi wao ICC wanataka Bara la Afrika liwakingie kifua, wakati Afrika inawahitaji walikuwa wako busy na Wazungu, hivyo naishauri nchi yangu ya TanZania ingawaje mimi siyo muumini wa hii ICC lkn nisingependa TanZania yangu iunge mkono jitihada za Kenya dhidi ya ICC, wacha Wazungu wawafundishe somo, na bado Wazungu wako na ninyi muda mrefu sana ujao mpaka mje kutambua kwamba Mzungu siyo rafiki wa Mwafrika bali ni adui, moto unakuja mwakani 2017 kwenye uchaguzi wenu, hapo ndiyo mtamjua Mzungu ile ya 2007 ilikuwa cha mtoto!
Aisee mkuu nimepitia uzi wako kweli nimepata kitu,nimeelewa nini janja ya kenya na huu ni uzandiki ulio hai,kenya wamelikoroga wenyewe wacha walinywe na hayo mawazo ya kuwakataa icc ni ya kipuuzi kabisa kwani kwa mfumo wa utawala wa kiafrika bila icc ndio afrika itajaa ma dikteta kuliko hata kina Hitla na Idi amini
 
Nakubaliana na wewe kwa 120%. Wakenya ni wabaguzi sana na wanajipendekeza sana kwa Wazungu pia hawakuwa na muda na kuipigania Afrika. Ni muda sasa wa kuwaacha kivyao wapambane na hao wazungu waliokuwa wanawalamba miguu kipindi Nyerere akiwa busy kupambana na makaburu.
 
Binafsi naiunga mkono ICC iendelee kuwepo. Regardless of its imperfections and partialities, still mahakama hiyo angalau inasaidia sana kuwatia adabu hawa wakoloni wa kiafrica. Hii mahakama kwa kiasi fulani ina-inject some elements of 'fear' kwa hawa viongozi wetu wa Africa ambao the majority wanajiwekea mazingira ya kubakia madarakani milele huku wakigandamiza wananchi.

Hakika nakuambia... if AFRICA will succeed to massively withdraw from ICC, basi wananchi watauawa kama njige. There will be more killings in Africa by its own leaders. Without ICC in place, the black continent is much likely to become a battle ground for civil wars.

However, sidhani kama wataweza kushindana na wazungu. Watabanwa tu na watatulia. It is a matter of time!

- Kaveli -
 
Umenena kweli. Lakini ni vizuri hata Waafrika wakawaida wakaacha kuitikia miiito kwa vibwagizo kufuatia propaganda za viongozi.

Hivi wakenya wanajiondoa ICC kwa maslahi ya Wakenya wenyewe au ni kwa maslahi ya kina laila, uhuru na wenzao?

Ninashangaa sana leo kenye wamesahau vile walichinjana kwa ajili ya upumbavu wa kfuata mikumbo ya miongozi mibinafsi bila maslahi yoyote. Ni jambo lisiloingia akili maika hii michache uchungu wa ndugu zao waliokufa umekwisha sasa hawataki hta vyombo vya kimataifa vifuatilie misingi ya uharifu huo ili hao mabwanyeye waliopelekea umwagaji damu wa andugu zao waadibishwe.

Burudni leo wanachinjana kwa sababu ya nkurunziza. Ajabu wakijiondoa ICC ili huyu muuaji ambaye hawana uwezo wa kumfanya kitu wao kama warundi asije kuchukuliwa hatua. Kwa hiyo wanabariki umwagaji damu wa ndugu zao usio kuwa na tija yoyote kwa taifa zaidi ya viongozi washenzi wala watu.

Kongo leo Kabila kaamua tu kuahirisha uchaguzi eti taifa halina fedha. Mifano ni mingi tu ya mitawala ya Afarica isiyofuata katiba za nchi na imetawala kwa nguvu na kusababisha umwagaji damu wa kutisha kndani ya mipaka yake. Nitashangaa iwapo kuna mraia wa kawaida ataunga mkono hii miongozi ihalaishe kujiondoa ICC ili inyanyase raia na wanaoipinga kwa namna itakavyo kwa kujua hakuna pahala yatawajibishwa.

Icc iko kwa kuthibiti uchafu wa viongozi wanaojimilikisha nchi na damu za wananchi wasiokuwa na mtetezi wala dola. Kama kuna mambo ya kurekebisha, ningeomba yawekwe bayana na yapendekezwe kama maboresho ili tuendelee kuyadhibiti haya madudu yanayotawala bila dhamira wala utu.

Kinyume cha pale, itakuw akama katiba ya tanzania, eti tume ikishatangaza raisi hakuna chombo cha kuchunguza utangazaji ule. Foolish!.
 
mkuu umeongea maneno kuntu tupu. Thumb Up for such great insights.

Mimi pia nawashangaa sana raia wa africa wanaounga mkono hiyo ajenda ya mitawala ya Africa kujiondoa ICC. Sasa hivi penyewe mitawala yetu ya Africa inaua innocent citizens bila huruma, what the situation would be if they become untouchable by the ICC ? Hell on earth !
 
Aisee mkuu nimepitia uzi wako kweli nimepata kitu,nimeelewa nini janja ya kenya na huu ni uzandiki ulio hai,kenya wamelikoroga wenyewe wacha walinywe na hayo mawazo ya kuwakataa icc ni ya kipuuzi kabisa kwani kwa mfumo wa utawala wa kiafrika bila icc ndio afrika itajaa ma dikteta kuliko hata kina Hitla na Idi amini
Hujamsoma vizuri pale aliposema hata yeye si muumini wa ICC.

Kikiumana pale Zanzibar utamsikia atakavyoikandia ICC, coz kina Nkapa na Magu hawatapona
 
mkuu umeongea maneno kuntu tupu. Thumb Up for such great insights.

Mimi pia nawashangaa sana raia wa africa wanaounga mkono hiyo ajenda ya mitawala ya Africa kujiondoa ICC. Sasa hivi penyewe mitawala yetu ya Africa inaua innocent citizens bila huruma, what the situation would be if they become untouchable by the ICC ? Hell on earth !
Mkuu ujue hakuna muuwaji anayeweza kujiua mwenyewe,hivyo basi hao viongozi wa afrika hawawezi kamwe kuipenda icc kwaniwanaelewa ndio kitanzi chao
 
Watapata supporters coz viongozi wengi wa Africa hawaipendi ICC kutokana na inavyowanyoosha.
Wananyooka kweli mkuu si unakumbuka elbashiri alivyo toka mkuku kule south kwa kukimbia order ya kukamatwa toka icc na kuwaacha viongozi wenzake wakila bata
 
Ilikuwa rahisi kujiunga na icc lakini kujiondoa sidhani kama azimio la au kutakiwa sababu tosh. Kila itakayotaka kuondoka itabidi itie notisi ya mwaka hivi na sababu zake. Sasa tukumbuke kuwa nchi nyingi za afrika zinategemea misaada hata Kulipa mishahara. Sasa Wakubwa wakitishia kusimamisha misaada kama nchi inaendeleza ajenda y kujitoa tutafanyaje.

Hili ni suala la kisheria na Kenya inijenge tu hoja nzito na luto atakuwa huru tu. Wapo wanaodai kuwa kwa siasa za kenya, bwana ruto anaelekea kuachwa kukaangoni huko the Hague. Ikiwa hivyo, wakalenjin wataamini wamechuuzwa. Kwa hiyo suala hili ni pana kuliko tunavyodhani. Ngoma ni nzito na hasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa 2017 huko Kenya.
 
Wananyooka kweli mkuu si unakumbuka elbashiri alivyo toka mkuku kule south kwa kukimbia order ya kukamatwa toka icc na kuwaacha viongozi wenzake wakila bata
Nakumbuka alikimbia haswa ila atakamatwa tu taratibu.

Atapewa hata 30yrs za kujifichajificha lkn atakamatwa na atashitakiwa.
 
Na huo ndio mara nyingi mwisho wa viongozi wengi wa nchi za kiafrika
 
Hapo ndipo ninapojiuliza hawa viongozi wa Africa wanajuaga wanachokifanya ktk uongozi wao au hawajielewi?

Unatafuta uongozi baadae unanogewa unataka kukaa kwenye uongozi milele unaanza kuuwa watu mwishowe unafungwa maisha, sasa ndiyo wanachokitafuta au ni nini wanatafuta?
 
Ni laana ya damu za watu mikononi mwao
 
Back
Top Bottom