Afrika inalala tena?

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,589
1,679
Kila mtu mwenye akili timamu anajua fika kwamba dunia inajiandaa kwa vita vya tatu vya ulimwengu. Ukifuatilia choko choko za Marekani dhidi ya Urusi na kutawanya kwake makombora katika bara Ulaya, ukifuatia kujipanua kwa Uchina kijeshi na kuunda zana mpya ziwe za anga au za maji.....India nayo haikuachwa nyuma, kila mara inaibuka na majaribio haya au yale ya silaha.
Ukienda Marekani ya Latino hali ni hivyo hivyo: Argentina na Brazil zinaongoza katika matayarisho.
Isipokuwa Afrika tu. Inaelekea Mwafrika hana mipango ya baadaye, haoni, hanusi, hasikii. Aidha, Waafrika wengi, ingawaje hakuna bara lililoteswa zaidi na watu weupe kama Afrika (biashara ya utumwa pekee imemaliza roho za Waafrika milioni 20, vita vilivyochochewa na nchi za Magharibi tangu 1960 huenda vimeteketeza roho nyingine milioni 20 -ukitazama Congo pekee watu milioni 5-6 wameteketea tangu 1995), bado wana imani kuwa kwa vile ni wanyonge basi vita vikija hawataguswa! Kuna wengine, kama mheshimiwa, bado wanawaangalia hawa jamaa kama baba na mama zao: mama hawezi kumtesa mwanaye!
Kama Waafrika wangekuwa wanasoma historia na kutosahau haraka, basi wangekutana upesi Addis Ababa kuzungumzia tu juu maandalio ya vita vya tatu kama bara moja!
 
Back
Top Bottom