Afrika inahitaji umoja

Afrika inahitaji umoja

Deinstein 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
2,087
Reaction score
3,916
Habari wakuu!

Kama kichwa cha uzi kilivyojibainisha ukweli ni kuwa Afrika bado haina Umoja. Sote tunajua wanaharakati kama Kwame Nkurumah walihubiri kuhusu hili ila bado juhudi zao hazikuzaa matunda stahiki.

Nasema hivi kwakuwa mataifa ya Afrika yamekuwa hayategemeani. Leo hii nchi ya Afrika ikivamiwa tegemea zaidi ikasaidiwa na vikosi vya UN au vikosi vya jeshi vya nchi ya Ulaya kama Russia au Ufaransa. Na hapo sijazungumzia issue za ukabila na migawanyiko inayotokana na vyama vya siasa.

Na ninaposema Afrika iwe na umoja simaanishi mataifa yote yaungane liwe taifa moja. La hasha, ila naamisha mataifa ya Afrika yategemeane na yashirikiane katika baadhi ya nyanja.

Moja ya nyanja hiyo ni defence yaani ulinzi. Mataifa ya Afrika yanatakiwa yaungane yatengeneza military research centre ambayo itasaidia kusoma mifumo ya ulinzi duniani kote na pia itasaidia kudevelop silaha za kijeshi zinazoendana na dunia ya sasa. Tunatakiwa tuache kuagiza silaha kutoka nje na kutengeneza silaha zetu wenyewe zitakazokidhi mahitaji ya sasa ya defence.

Nyanja nyingine ni health sector. Kumekuwa na magonjwa yakilipuka Afrika kama vile M pox lakini cha kushangaza tunasubiri wazungu watutengenezee dawa na chanjo inhali sisi tuna madaktari na mafamasia wa kutosha.

Mataifa ya Afrika yanatakiwa yaungane yatengeneze medical research centre ambayo itawezesha kutokomeza magonjwa yanayoisumbua Afrika kama Malaria na tuache kutegemea dawa kutoka kwa wazungu.

Pia bunge na mahakama ya Afrika inatakiwa ikemee maovu na ufisadi unaofanywa na viongozi wa Afrika. Lissu kafungwa jela bila sababu inayoeleweka nashangaa kuona bunge la EU ndo linalaani hii kitu wakati bunge la AU lipo kimya. Hata mgogoro unaotokea kule South Sudan bunge la AU halijatoa tamko lolote kuhusu hilo.

Kwa kumalizia, kuna msemo unasema ukitaka kwenda mbali kwenda na wenzako, ukitaka kufika haraka nenda peke yako. Mataifa ya Ulaya yamedhihirisha huu msemo kutokana na EU. Leo hii mwingereza anaweza kwenda Ufaransa na akafanya shughuli zake bila shida yoyote. Hata amani katika bara la Ulaya umeongezeka sio kama hapo mwanzo enzi za WWI na WWII.

Hata UAE imedhihirisha hili state zake kama vile Dubai zimepiga hatua kubwa mno.

Yangu ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom