Afrika Hakuna Tena Viongozi

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,271
4,633
nashawishika kuandika maneno haya kwa uchungu mkubwa nikikumbuka jinsi afrika ilivyopata kubarikiwa kuwa na viongozi ambao wengi wao walijitoa muhanga kuhakikisha bara linarudishwa mikononi mwa wazalendo na kuhakikisha wanauvurumishia mbali utawala wa mkoloni.

kumbukumbu zisizosahaulika zinaonyesha wazi kuwa afrika ilikuwa inatawaliwa na wakoloni ambao waligawana nchi kama vile wanagawana nguo za marehemu. lakini mwisho wa siku kuna watu ambao sisiti kuwaita mashujaa ndio walipambana kwa mtutu wa bunduki au kwa njia ya majadiliano mezani na kupelekea nchi nyingi kupata uhuru. na kama hiyo haitoshi viongozi hawa walifanikiwa kujenga umoja na mshikamano baina ya waafrika na kujenga misingi ya kujitawala wenyewe bila kuendeshwa na wakoloni. viongozi wengi waliopambana na wakoloni walikataa kubuluzwa na kupelekwa wasipojua na wakoloni. pia kila kiongozi alihakikisha kuwa kila mali iliyopo katika nchi ni mali ya wazalendo na inamilikiwa na wazalendo.sintakuwa mwenye busara kama sitowaorodhesha baadhi kati yao, na wengi wao kwa sasa hatunao tena duniani.

miongoni mwao walikuwepo kina kwame nkurumah, stiven bicco, mandalane, patrice lumumba, gamal abdul massa, joshua nkono, robert mugabe, mutaala, kanaan banana, jomo kenyata, kamanda samora machel, keneth kaunda, nelson mandela, muamal gadaffi, haile selassie na kwa kiasi fulani naweza kumuweka kambarage nyerere yule wa miaka ya sitini. hawa ndio waafrika ambao walipambana kwa ajili ya afrika na mwafrika.

afrika ya sasa imekuwa na viongozi tofauti na hao niliowazungumzia hapo mwanzo, afrika imekuwa na viongozi wenye kila aina ya kashfa katika jamii, afrika imekuwa na viongozi wala rushwa, mafisadi, wanaotumia mali ya taifa kwa manufaa yao wenyewe, wasiojua utawala bora, wasio na uchungu wa kuona mali za wazalendo zikitafunwa na wachache, waoga kutoa maamuzi au hata kukemea uovu, wasiotenda mema yanayokwenda sawa na nyadhifa walizokabidhiwa, wenye kutetea uovu unaofanywa na washirika wao, wenye kung'ang'ania madaraka, wezi wa kura na wasioingia madarakani kwa kura halali na madhambi mengine meengi ambayo naona hata kichefuchefu kuyaorodhesha.

Miongoni mwa hayo tunayaona yakituzunguka katika bara la afrika. imefika kipindi nawaza kuwa je kama viongozi hawa wanaotawala sasa wangekuwepo kipindi kile nchi nyingi za kiafrika zilikuwa zinadai uhuru je wangeweza kupambana na mkoloni au wangekaa chini na kufanya makubaliano ya kuuza kila kilichipo katika nchi kama wanavyofanya sasa kisha wao, famila zao na washirika wao wangetimkia ughaibuni na kutuacha hatuna mwelekeo?

Hapo ndipo nalazimika kusema wazi kuwa afrika ya sasa imekosa viongozi.


nawakumbuka sana viongozi ambao tuliofanikiwa kuona utendaji wao tunaamini kuwa walishushwa kutoka mbinguni ili kuja kuliinua taifa la tanzania nao ni seti benjamin, dr kleluu na edward moringe sokoine, kwani kama hawa wangekuwepo basi ni wazi kuwa kwa kipindi chote ambacho walikuwa madarakani tanzania ingepata maendeleo makubwa na wangejenga mwongozo mzuri wa utendaji wa kazi na tungekuwa tunapata viongozi bora kutokana na kuvaa viatu vya waheshimiwa hao. ni wazi kuwa tokea mwenyezi mungu awachukue viongozi hao tanzania haijapata tena viongozi bora bali watanzania wanapata bora viongozi ambao mwisho wao ni kuwaacha wazalendo wakiwa katika maisha magumu na ya aibu kwa taifa lililoojaaliwa na mwenyezi mungu au la waturudishe mikononi mwa wakoloni...
 
Miaka hamsini zaidi ya utawala wa mkoloni ungejenga viongozi na taasisi imara zaidi. Utawala wa mswahili unatia aibu. Mwenye macho haambiwi ona.
 
Ni kweli mkuu, chini ya utawala wa mswahili, polis wanaua raia hovyo badala ya kuwalinda! Afadhali mkoloni mweupe, kuliko mkoloni mweusi.
 
Mfano mzuri waingereza wametoka Hong Kong miaka ya themanini na kuacha mafanikio makubwa kimaendeleo.
 
Misingi ya ukoloni ingekuwa ni matumizi ya raslimali zetu kwa maendeleo yetu, ningekubali. Lakini sio wizi wa raslimali zetu kwenda kwao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom