African 'one term' presidents: Will Samia take a course?

African 'one term' presidents: Will Samia take a course?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,144
Reaction score
56,413
Mwaka 2018 miaka mitatu kabla ya kifo cha hayati Magufuli niliandika makala hii ndani ya JF "African 'one term presidents : Will Magufuli take a course?"

Leo tena nakuja na makala fupi inayofanana na hiyo kutokana na hali ya kisiasa ilivyo nchini.

Mimi sio mtabiri bali huwa nalinganisha matukio ya sasa na yaliyopita kwa ufanano wake na kuja na conclusion, kwa waliosoma logic wanajua, 'if this.... then..... '.

Kifupi, Afrika ina marais waliokaa madarakani kwa muda mrefu aidha kwa kupendwa na wananchi au kwa mabavu kama, Yahya Jammeh wa Gambia, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Paul Biya wa Cameroon, Yoweri Museven wa Uganda.

Kuna wale waliodumu kwa vipindi vifupi hadi siku 2 tu au muhula mmoja (one term president) na kuondolewa madarakani kwa sababu mbalimbali, mfano,

Christopher Elnathan Okoro Cole wa Sierra Leone aliapishwa kuwa Rais na baada ya siku 2 akajiuzulu.

Yusuf Kironde Lule wa Uganda alikuwa rais wa Uganda kwa siku 68 tu. akaondolewa na bunge.

Robert Guei – Ivory Coast alikuwa rais kwa miezi 10, akashindwa uchaguzi.

Michel Djotodia alikuwa rais wa Central African Republic kwa miezi 9, akaondolewa na Baraza la Usalama UN.

Ernest Adegunle Oladeinde Shonekan alikuwa rais wa Nigeria kwa miezi 3 tu, akalazimishwa kujiuzulu na wananchi kwa maandamano.

Tito Okello alikuwa rais wa Uganda kwa miezi 5 tu, Aliondolewa na waasi wa NRM chini ya Yoweri Museveni.

Thomas Sankara wa Burkina Faso aliingia madarakani mwaka 1983 kwa mapinduzi ya kijeshi, October 15, 1987 aliuawa na wajeshi.

Rais Melchior Ndadaye wa Burundi, alidumu madarakani kwa miezi 3 tu, aliuawa na wanajeshi wa Kitusti.

Rais John Joseph Magufuli wa Tanzania aliongoza kwa muhula mmoja na nusu, alifariki kwa matatizo ya kiafya.

Rais Mohamed Morsi wa Misri aliingia madarakani 2012 baada ya nguvu ya umma kumwondoa dikteta Hosni Mubarak, waliamini labda Morsi atakuja kuwa kiongozi mzuri kwao.

Baada ya Morsi kupewa madaraka alibadili katiba na kujipa madaraka yote, kila kitu aliamua yeye bila kulihusisha bunge, mahakama wala vyombo vya sheria. Aliwakamata na kuwaua wote waliokuwa wakimpinga.

Kutokana na utawala wake wa mabavu wa kutofuata sheria Morsi alishitakiwa kwenye Mahakama ya nchi hiyo na May 2015 alihukumiwa kunyongwa.

Tuna cha kujifunza kutokana na utawala huu wa Samia?

na Quinine wa JF.
 
Kwa hiyo mlimuua Magufuli mkitegemea nchi itayumba?
 
Back
Top Bottom