Binafsi nimefanya Environmental and Social Impact Assesment (ESIA) kwenye huo mradi upo katikati ya vilima viwili Ngasamo upande wa Magu na Mang,ola upande wa Bariadi na mradi wenyewe uliitwa Dutwa kwa sababu Dutwa ni centre ya karibu kutoka hapo kwenye project area.
Lakini pamoja na Cobati, pia pembeni ya mlima wa Ngasamo kuna wachimbaji wadogo wadogo wa gold, hofu yangu ni kuzuka kwa mgogoro, kwani wakati ESIA, niliona viongozi wengi wa serikali wakipendekeza wachimbaji hao waondolewe, na nilipojaribu kuongea na hao wachimbaji walisema hawako tayari kwani wana vibali vyote.
Kwa taarifa tu wakenya pia wanaandaa ujenzi wa siri wa reli toka Sirari mpaka Nairobi kuunganisha reli ya Mombasa ku win biashara ya Nickel kwa sababu reli yetu ya kati imekufa.