African Democracy

Nini Maoni yako juu ya kuwa na African Democracy?

  • Iwepo

    Votes: 1 100.0%
  • Isiwepo

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    1

Kishoka2

Member
Aug 23, 2017
16
13
Demokrasia ni hali ya watu kuwa huru kuchagua au kuchaguliwa, kuwasilisha maoni binafsi kwa mujibuwa sheria bila pingamizi, uhuru wa kuchagua itikadi ama dini nakadharika.

Kwa kiasi kikubwa bara letu la Afrika limekuwa likifuata demokrasia ya kimagharibi. Misingi ya demokrasia hii ya kimagharibi imeasisiwa hukohuko magharibi chini ya misingi ya kitamaduni ya kimagharibi.

Demokrasia hii inataka "Majority rule" katika misingi ya kuwa wengi watashinda.

Nini Madhara/Athari ya Demokrasia hii ya kimagharibi?
Athari ya moja kwa moja ya demokrasia hii ni itikadi ya wengi washinde, katika dhana hii si ajabu tukashuhudia mambo yaliyokuwa "Mwiko" ama aibu kufanyika katika jamii zetu yakiwa ya kawaida kabisa. Mfano hali ya vijana wengi kujiingiza katika ushoga ni matokeo ya muingiliano wa kijamiii, kiteknolojia na kiuchumi na mataifa mengine. Katika hali hii vijana wetu wengi wameathirika na tatizo la ushoga na sasa shoga anaweza kujiweka hadharani bila shaka wa woga. Mashoga wakiwa wengi nchini, chini ya demokrasia hii ya kimagharibi hakuna shaka ipo siku ushoga utaruhusiwa kwa ndoa halali za kiserikali. Huu ni mfano mmoja tu, ipo mingi juu ya athari za kimagharibi tunazozikumbatia.

Kwanini African Democracy?
Kihistoria hasa nikichukulia historia ya chaguzi za viongozi wa kichifu, ilikuwa viongozi wanapatikana kutokana na mchakato wa kupima uwezo wa muhusika katika maeneo mbalimbali. Mfano kiongozi wa kijadi katika kikosi cha kivita alipatikana kwa kupima uwezo wake katika mbinu za kivita na kimapigano. Leo tunachagua majemedari kutokana na elimu zao za darasani, vivohivyo viongozi wa kijadi wamekuwa aidha wa kurithi kwenye ukoo au familia inayofahamika kwa uwezo wake wa kuongoza. Hiyo ndio ilikuwa njia ya kuwapata viongozi katika maeneo mbalimbali ya kiutawala. Leo hii kwa demokrasia hii usishangae hata shoga akawa kiongozi, ni hatari.

Hii ndio maana nasema tunahitaji kama bara, kuwa na demokrasia yetu inayorandana na tamaduni zetu kama waafrika. Naamini tukiwa na demokrasia yetu wahunzi na wafinyanzi waliokuwa na vipawa hivyo watapatikana na kuamsha uchumi wetu wa kiafrika.
 
Back
Top Bottom