mchinja kobe
Member
- Dec 20, 2012
- 8
- 2
Naam wanajamvi....
Leo nakuja na uzi juu ya mwenendo wa nchi zetu za Africa hasa Tanzania taifa langu, ukifuatilia kwa ukaribu mwenendo wa nchi karibu zote za Africa hasa za Africa magharibi na zote za kusini mwa jangwa la sahara utagundua kuna vitu tunashare in common as Africans, kuna majibu mengi yaliyotolewa na yanaendelea kutolewa na wasomi, wanasiasa na watu mbali mbali juu ya nini kifanyike ili mataifa yetu yaendelee, na ukichunguza kwa umakini majibu karibu yote kuna namna yanafanana, hata leo ukiulizwa nini kifanyike kwa mataifa yetu majibu yako hayatakuwa na utofauti mkubwa na yale ambayo huwa yanatolewa na hata viongozi wetu wanayafahamu vema, kwa mtazamo wangu tatizo mojawapo kubwa linalosumbua nchi zetu za Africa.
Tanzania ikiwa miongoni, ni ukosefu wa TAASISI IMARA (strong institutions), TAASISI namaanisha sheria zetu zinazovipa mamlaka-(mandate/authority), vyombo vyetu vya kuendesha nchi, mfano (Tanzania) Usalama wa taifa, TAKUKURU, Polisi, Sumatra, TRA, Rais, Bunge, Mahakama, PPRA, NEC na vingine vingi, sheria zetu zinazounda vyombo hivyo na vyombo vyenyewe pamoja na sheria mbali mbali zinazosimamia mwenendo wa uendeshaji nchi kwa kila mTanzania kwa nafasi yake, kwa kueleza hayo nadhani KATIBA yetu ya sasa inayo madhaifu sababu hasa ndiyo mama inayopelekea kuzaliwa kwa sheria nyingine zote.
Ukienda kwa vyama vya siasa (upinzani) wanalalamika juu ya tume ya uchaguzi hadi imefika watu wanawachukia watendaji wa tume ya uchaguzi na ukienda kw watendaji wa tume watakueleza madhaifu hasa ktk mamlaka (mandate) kama taasisi, ukienda kwa polisi ukiwalalamikia nao pia wana tatizo la mandate wapi wanaanza na wapi wanaishia na mipaka ya kuingiliwa na vyombo vingine vya juu au watu wenye mamlaka ya juu, hali ni vivyo hivyo kwa Usalama wa Taifa, mahakama, Bunge na vyombo vingine, kwa TAASISI (institutions) tulizonazo sasa zinatoa mianya mingi kwa watu "HASA WENYE MAMLAKA" karibu kila ngazi ya uongozi na utendaji kuweza kuingiza maslahi binafsi, maslahi ya mtu fulani au ya kikundi fulani au hata kupindisha sheria ktk namna itakayo faa kwa mtazamo wake au wao wala si kwa maslahi ya wote kama Taifa.
Unaweza kuona mfano wa sheria ya manunuzi ya umma iliyobadilishwa inayoruhusu serikali kununua vitu "USED", mamlaka makubwa sana ya rais, sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi, sheria ya uhuru wa vyombo vya habari na sheria nyinginezo nyingi ambazo zote zinapelekea uwepo wa watendaji na viongozi wabovu, wenye maslahi binafsi na mara nyingi ukipata sheria zisizo na tatizo basi nyingi hazina maslahi ya moja kwa moja au hazina kabisa maslahi kwa viongozi au watendaji. Jibu ambalo limekuwa likitolewa kama sababu ya kukwama kwa mambo mengi ktk nchi zetu hasa ni "UKOSEFU WA UTASHI WA KISIASA" (lack of political will) na hilo lina ukweli kwa kiasi kikubwa katika kuchangia uwepo wa TAASISI lege lege na mbovu za kuendesha Taifa chini ya taasisi mbovu inahitaji UTAIFA na USTAARAB wa mtu mwenyewe kujiepusha na matumizi mabaya ya madaraka au nafasi ya umma, nadhani ni wakati muafaka sasa sote kama TAIFA na (ieleweke kwamba TAIFA ni zaidi ya makabila, Dini, itikadi za kisiasa, rangi, kanda, na tofauti nyingine zote tukiwa TAIFA sote ni wamoja), kwa fursa hii ya katiba mpya na kila mmoja kwa nafasi yake kufikiria kuhusu mustakabali wa TAIFA letu kwanza na vizazi vyetu vijavyo japo kuna mengi ya kukatisha tamaa na kurudisha nyuma lakini tukiamini katika kitu kinacho tuunganisha UTAIFA wetu wote tutafanya maamuzi sahihi na yenye maslahi kwa taifa kila mtu kwa nafasi yake Rais, muuzaji wa karanga, mkulima, mbunge, mwalimu na wote tutimize wajibu wetu kama WATANZANIA.
Ni matumaini yangu na ndoto ya kila Mtanzania kuwa na TAIFA lenye maendeleo, ustaarab, kuheshimiana, kuvumiliana, na TAIFA lenye heshima kutokana na kujali utu, Hapa ndipo linakuja suala la VIONGOZI kusimama kwa nafasi zao na MAMLAKA yao ili kujenga TAASISI imara zitakazoruhusu kila MTanzania mwenye uwezo kulitumikia TAIFA kwa ufahari bila akijua anajenga TAIFA, wajibu wa viongozi ni mkubwa na hapa ni viongozi wa ngazi zote za taifa hili pamoja na mwanachi mmoja mmoja kwa nafasi yake.
Tupiganie kujenga nchi yetu yote mabaya yanayotokea tuyachukulie kama changamoto ambazo zinahitaji ufumbuzi ili kufikia Tanzania ambayo wengi wetu tunapeenda iwe. Tuanze sasa kwa kujenga TAASISI IMARA za kuongoza TAIFA. Naiona TANZANIA yenye neema ikiwa mioyoni mwa WATANZANIA ni veme tuipiganie sasa kama WATANZANIA, bila kujali tofauti zetu.