Afisa wa kijeshi ahamia Korea Kusini

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,432
8,140
ImageUploadedByJamiiForums1460546322.266274.jpg

walinzi wa mpaka nchini korea kaskazini

Afisa wa kijeshi wa cheo cha juu nchini Korea Kaskazini, ambaye alikuwa akisimamia masuala ya ujasusi ameihama nchi hiyo na kuelekea Korea Kusini.
Afisa huyo hajatajwa jina lakini wizara ya ulinzi nchini Korea Kusini inasema kuwa alikuwa afisa wa cheo cha juu na aliondoka nchini Korea Kaskazini mwaka uliopita.
Shirika la habari la Yonhap nchini Korea Kusini, lilinukuu taarifa zilizosema kuwa kanali huyo alitajwa kuwa shujaa na wale walioihama Korea Kaskazini.
Maelfu ya watu kutoka Korea Kaskazini wamehamia nchini korea Kusini tangu vimalizike vita vya Korea
Zaidi ya watu 28,000 wameihama Korea Kaskazini tangu kumalizika kwa vita vya Korea, lakini kuhama kwa maafisa wa vyeo vya juu si jambo la kawaida,.
Wiki iliyopita raia 13 wa Korea Kaskazini waliokuwa wakifanya kazi kwenye mikahawa nchini humo, walihama kwenda Korea Kusini kwa pamoja.
Shirika la Yonhap linasema kuwa wanasiasa kadha wa vyeo vya juu wamehama kwenda Korea Kusini siku za hivi majuzi wakati wakifanya kazi nchi za ng'ambo.
 
Back
Top Bottom