Afisa Misitu wilaya ya Mpanda ni Mungu Mtu

Afisa Misitu wilaya ya Mpanda ni Mungu Mtu

odeyo

Member
Joined
Apr 4, 2013
Posts
8
Reaction score
1
Kwa masikitiko makubwa napenda kuufahamisha umma wa watz, tabia za Afisa huyu ambae kwa kweli anacheza na mitaji yetu wafanyabiashara wa mazao ya misitu tunaofanya biashara katika wilaya hii.
Kwa makusudi kabisa hataki kuitisha kikao cha wilaya cha kujadili maombi ya leseni. Tumetuma maombi hayo tangu mwezi Julai mwaka jana, tumelipia usajili hadi sasa unakaribia kuisha mwezi june mwaka huu. Kibaya zaidi tunapompigia kuuliza ni lini anatujibu vibaya kwa kejeli na dharau.
Kabla uvunaji ulikuwa unasimamiwa naye mambo yalikuwa yanaenda vizuri, pesa ikitumwa toka wizarani anatutaarifu pesa tayari leteni maombi. Sasa pesa ipo lakini haiti vikao kwa kuwa wizi alokuwa anafanya na baadhi ya wafanyabiashara sasa hivi amedhibitiwa. Rungu liko na watu wa wizara husika. Matokeo anatutesa wafanyabiashara ambao tunalipa kodi zetu na zimeenda bure. Afisa huyu amesababisha wafanyabiashara wengi sana kukimbia mpanda kutokana na ubabe wake. Ana wafanyabiashara wake ambao imefika mahali anapanda malori yao yenye mbao na kuwasindikiza hadi Sumbawanga wakiwa hawana vibali, yeye ndio anakuwa kibali. Pia anatumia watumishi walio chini yake kutunyanyasa wafanyabiashara, mfano kuna mfanyakazi alimwachia ofisi kipindi yupo masomoni katusumbua na kutufilisi sana pale tulipokataa kutoa pesa za kumpa ampelekee bosi wake. Uongozi wa mkoa wa katavi unalijua hili ila unalifumbia macho, kwa kuwa tumepeleka sana malalamiko kwa mkurugenzi wa Halmashauri wa kipindi cha nyuma ambae sasa hivi ni RAS wa Katavi. Lakini hajafanya lolote. Hivi nchi hii tutawaabudu watu kama hawa hadi lini? Huyu ni mtu mdogo sana hawezi kusema ana kazi nyingi kipindi chote cha miezi takriban kumi. Kama kabla ilikuwa inawezekana, kwa nini sasa hivi inakuwa ngumu?
 
mmh!poleni wanyonge wenzangu,kwani hapo inatuweka wazi kuwa wenyenchi wanalitambua ila wanabebana kutuumiza wanyonge.

hayo ndiyo maisha bora !,ila wakati utafika.

hakuna marefu yasiyo nancha.

poleni saana.
 
Hiyo ndiyo faida ya serikali legelege ya mtukufu wetu mzee wa anga full time hivi amefikisha safari ya ngapi juu ya anga?
 
katavi mnani? juzi kuna madiwani wanataka kumng'oa mkurugenzi leo afisa misitu ni nini kinachoendelea????
 
ni ubabe ambaao hauna maana ndo maana mkoa haendelei,full magumashi kila kitu..
 
Mkuu kwa ufaham wangu najua anayepaswa kuitisha kikao cha uvunaj ni mwenyekit wa uvunaj wilaya ambae ni dc,ye afisa misitu ni mjumbe tuu,lawama zote apewe dc,vp huna namba ya mgoo?
 
Dc haujui mninga wala mkongo jamani, ded ndio katibu na afisa misitu ni mwajiriwa wa ded, yeye ndo anahusika moja kwa moja kumkumbusha juu ya umihimu wa kuwepo kikao hicho. Huyu anawajibika mwenyewe moja kwa moja, na ndio maana pesa za kikao hicho hupitia kwa Afisa Misitu. Na hata maombi hayo ya kuvuna leseni hutumwa kwa Afisa Misitu. Hana pa kukwepea, unless atoe sababu za yeye kutosimamia uwepo wa kikao hicho.
 
Tatizo wafanyakazi wa mikoa ya pembezoni huwa wana ubabe usio na maana. Hudhani kila mtu ni mbumbumbu. Ofisi zinaendeshwa kama vile ni ofisi zao binafsi tena za vilabu vya pombe za kienyeji. Badilikeni, ubinafsi wenu utasababisha mkoa kupiga hatua mbele hatua nyuma. Tumikieni wananchi msijisahau sana.
 
Back
Top Bottom