Afisa Elimu Nyamagana Anadumaza Elimu.

serengo

JF-Expert Member
Jul 30, 2013
488
362
Kumekuwepo na Tabia ya kushusha walimu wakuu ( Msingi) vyeo katika Wilaya ya Nyamagana - Mwanza.Kazi hiyo hufanywa na Afisa elimu Wilaya akishirikiana na waratibu elimu Kata,sababu kubwa ni kwa ajili ya kuwatafutia watu wao ukuu.
Ila jambo hilo LA kuwavua walimu wakuu madaraka linafanyika kwa uonevu sana na kuharibiana CV, mfano Mwalimu amepewa ukuu January 2017 then February 2017 unamvua madaraka ? Ulitumia kigezo gani kumupandisha kuwa mkuu na umetumia vigezo gani kumvua? Huu ni uzalilishaji sana na inatokea sana kwa watu ambao hawana Wa kuwatetea hapo Jiji,
Vigezo vikuu wanavyotumia kutafuta magep hayo ni
I. Shule kutofanya vizuri kwenye mitihani.umenipa shule January umenitoa February ni mtihani gani ambao umefanyika hapo katikati?Hiyo ni njia moja wapo ya udhalilishaji.
Ii.Sababu ya Pili mwalimu mkuu kutowawajibisha walimu wachelewaji? Je ww afisa elimu ulishawahi kufika kwenye shule na kufanya ukaguzi kwenye daftari LA mahudhurio?,Ulitoa onyo lolote? Au afisa yeyote alishafanya ukaguzi kwa shule hiyo? Mkuu anashushwa cheo bila kufanyiwa ukaguzi wowote wala barua yoyote ya onyo, Tunaharibia CV kwenye file zetu jamani.
Ninaomba uongozi Wa mkoa uiangalie sana ofisi ya Afisa elimu Nyamagana, malalamiko ya unyanyasaji Wa walimu yamekuwa mengi, huyo afisa elimu aliyepo hafai hata kwa dawa, ataharibu taaruma ya nyamagana .
Uongozi Wa elimu mkoa Wa Mwanza umuchunguze vizuri anaharibu dira ya elimu nyamagana,maana anachangia sana udumavu Wa elimu kwenye Wilaya hii.
 
hua najiuliza. hivi katika semina zao elekezi, hua wanafundishwa kuhakikisha wanawanyanyasa walimu kwa kadiri ya uwezo wao?
inauma sasa pale unataka kujituma kwa manufaa ya taifa, huku ukiwa unateswa na kuzarauliwa na wale waliotakiwa kukupa ushirikiano.
kamshahra kenyewe kahovyo, mwalimu mwenye shahada kushidwa hata na polisi aliyefeli kidato cha nne; ila bado wanatuongezea na mateso.
 
Kwa kweli inaumiza sana kama ni hiyo posho ya madaraka inawafanya wawatafutie jamaa zao ukuu hatufiki popote juu ya elimu yetu, Mwl anafanya kazi kwenye mazingira magumu Afisa umutegemeaye naye anakunyanyasa ,,,kwa kweli walimu tunamzigo mzito sana
hua najiuliza. hivi katika semina zao elekezi, hua wanafundishwa kuhakikisha wanawanyanyasa walimu kwa kadiri ya uwezo wao?
inauma sasa pale unataka kujituma kwa manufaa ya taifa, huku ukiwa unateswa na kuzarauliwa na wale waliotakiwa kukupa ushirikiano.
kamshahra kenyewe kahovyo, mwalimu mwenye shahada kushidwa hata na polisi aliyefeli kidato cha nne; ila bado wanatuongezea na mateso.
 
tatizo kubwa wanafanya kazi kwakuiga viongozi wao wajuu kila afisa anataka awonekane kwakutumbua wanyonge ambao hawana mtandao juu wakuwakonecti tena sio shule za msingi tu hata sekondari hiyo tabia ni kawaida sanaa shule nyingi zimebadilishiwa wa kuu bila sababu za msingi zaidi ya (cheap popularity) ya viongozi wa elimu wa jiji. ukija katika sekita ya afya ni yaleyale ata bwana afya wa kata anafika wakati wote eti kukangua bila kufuata wataratibu anatamukatu kiasi chochote eti fine ya Kosa atakalo hisi kuwa kosa kwasababu alishaona kwenye runinga waziri anatoza fine. kwahiyo ni shida kubwa sana kwawale wasio kua na mtandao jiji.
 
Hiyo mihemuko yao inaharibu sana maono ya walimu maana unawekewa barua ya ajabu ajabu kwenye file ambayo itakuharibia future yako, Dawa ya Hawa ni kupambana nao kwenye ngazi za juu tu.Bora kulinukisha kuliko kuharibiana sifa .
tatizo kubwa wanafanya kazi kwakuiga viongozi wao wajuu kila afisa anataka awonekane kwakutumbua wanyonge ambao hawana mtandao juu wakuwakonecti tena sio shule za msingi tu hata sekondari hiyo tabia ni kawaida sanaa shule nyingi zimebadilishiwa wa kuu bila sababu za msingi zaidi ya (cheap popularity) ya viongozi wa elimu wa jiji. ukija katika sekita ya afya ni yaleyale ata bwana afya wa kata anafika wakati wote eti kukangua bila kufuata wataratibu anatamukatu kiasi chochote eti fine ya Kosa atakalo hisi kuwa kosa kwasababu alishaona kwenye runinga waziri anatoza fine. kwahiyo ni shida kubwa sana kwawale wasio kua na mtandao jiji.
 
tatizo kubwa ni kwamba kule ju kwa utawala hu kila mtumishi anafanya kazi kwa uoga wa hari ya juu fikra zao ni hofu ya kuwa next kwa kutumbuliwa kwahiyo hawataki kupambana nawatumishi wao wa chini ni wacheche wanao kuwa brave kurisiki na kuchukua hatua sitahili. subira ndo siluhisho la haraka tu watashidwa tu
 
Back
Top Bottom