Afariki baada ya kukusanya Sh2 milioni za msiba

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Moshi. Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya sheria aliyekusanya fedha kwa ajili ya msiba wa rafiki, amefariki kwa ajali ya gari jijini Nairobi, siku moja kabla ya mazishi.

Mwanafunzi huyo anayeitwa Glory Mbuya au maarufu kwa jina la Chuda na ambaye alikuwa maarufu katika miji ya Moshi, Nairobi, Arusha na mikoa jirani, alifariki dunia saa chache baada ya kumaliza sherehe yake ya siku ya kuzaliwa.

Taarifa za kufariki kwa mwanafunzi huyo, zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii jana, zikielezea namna ajali hiyo ilivyotokea.
Habari zinaeleza kuwa siku moja kabla ya kufariki dunia, alikuwa amechangisha zaidi ya Sh2 milioni za rambirambi kwa ajili ya kifo cha mke wa mfanyabiashara mmoja wa Moshi aliyezikwa jana.

Adamu Mushi, mmoja wa marafiki wa familia ambayo ilifiwa, alisema Chuda alikuwa anakuja mjini Moshi kushiriki mazishi ya mke wa mfanyabiashara huyoanayeitwa Wario Mushi.

Alisema Chuda alikuwa rafiki wa karibu na kijana wa marehemu ambaye walikuwa wakisoma wote.“Huyu dada alikuwa ni rafiki yake na mmoja wa vijana wa mama ambaye tunamzika leo (jana),” alisema.

“Japo tuko kwenye majonzi mazito ya mama yetu tumepata taarifa zake za ajali katika mitandao. Kwa kweli imetuumiza sana japo nasi pia tunaomboleza msiba wa mama.”

Gazeti moja la Kenya limesema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi baada ya gari waliokuwa wakitumia na wenzake kumgonga mtembea kwa miguu na hivyo kuacha njia na kupinduka likiwa Barabara ya Mbagathi jijini Nairobi.

Chanzo: Mwananchi
 
Rest in Peace, Chudah
IMG-20181212-WA0007.jpeg
 
Maskinii. Anaonekana alikuwa na roho ya upendo. Mwenyezi Mungu amtie kwenye nuru ya milele. Apumzike kwa amani Chuda!
 
Moshi. Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya sheria aliyekusanya fedha kwa ajili ya msiba wa rafiki, amefariki kwa ajali ya gari jijini Nairobi, siku moja kabla ya mazishi.

Mwanafunzi huyo anayeitwa Glory Mbuya au maarufu kwa jina la Chuda na ambaye alikuwa maarufu katika miji ya Moshi, Nairobi, Arusha na mikoa jirani, alifariki dunia saa chache baada ya kumaliza sherehe yake ya siku ya kuzaliwa.

Taarifa za kufariki kwa mwanafunzi huyo, zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii jana, zikielezea namna ajali hiyo ilivyotokea.
Habari zinaeleza kuwa siku moja kabla ya kufariki dunia, alikuwa amechangisha zaidi ya Sh2 milioni za rambirambi kwa ajili ya kifo cha mke wa mfanyabiashara mmoja wa Moshi aliyezikwa jana.

Adamu Mushi, mmoja wa marafiki wa familia ambayo ilifiwa, alisema Chuda alikuwa anakuja mjini Moshi kushiriki mazishi ya mke wa mfanyabiashara huyoanayeitwa Wario Mushi.

Alisema Chuda alikuwa rafiki wa karibu na kijana wa marehemu ambaye walikuwa wakisoma wote.“Huyu dada alikuwa ni rafiki yake na mmoja wa vijana wa mama ambaye tunamzika leo (jana),” alisema.

“Japo tuko kwenye majonzi mazito ya mama yetu tumepata taarifa zake za ajali katika mitandao. Kwa kweli imetuumiza sana japo nasi pia tunaomboleza msiba wa mama.”

Gazeti moja la Kenya limesema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi baada ya gari waliokuwa wakitumia na wenzake kumgonga mtembea kwa miguu na hivyo kuacha njia na kupinduka likiwa Barabara ya Mbagathi jijini Nairobi.

Chanzo: Mwananchi
RIP Chudda, mungu akuweke unapostahili
 
Back
Top Bottom