Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,874
- 7,650
Kuna uwezekano mkubwa mwanamuziki Selemani Msindi (Afande Sele) kuwa katibu mkuu wa pili wa chama cha ACT Wazalendo.
Hii inatokana na ukweli kuwa chama hicho kwa sasa hakina katibu mkuu baada ya Mwigamba kubwaga manyanga, na kukimbilia 'shuleni'.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wameeleza kuwa pamoja na Mwigamba kuagwa kwa sherehe lakini kumetokea sintofahamu ya ndani kwa ndani ambapo sasa chama kimegawanyika katika makundi mawili.
Lipo kundi tiifu kwa kiongozi wa chama ndugu Zitto Kabwe ambalo linaonekana halifurahishwi na 'cheo' alichojipa kiongozi huyo kwa hoja kwamba kinamshusha badala ya kumpaisha na kwamba Mama Anna Mghwira ambaye naye ana kundi lake anaonekana anang'aa na kumfanya aonekane ni bora zaidi katika kukiongoza chama.
Inaelezwa kuwa Mwigamba hamuungi sana mkono Zitto Kabwe na anapendelea zaidi mabadiliko ya katiba ili kuondosha cheo cha Kiongozi Mkuu wa Chama na kubaki na mwenyekiti tu.
Watu wa karibu na viongozi hao wamekiri kuwa kuna msuguano mkali ndani ya ACT wazalendo na Mwigamba ameamua kistaarabu 'kwenda kusoma' ili asiwe sehemu ya kuporomoka kwa chama ambapo sasa ni dhahiri kinaporomoka kwa kasi sana.
Katika kutafuta Mrithi wa Mwigamba, Selemani Msindi anatajwa kuwa na uswahiba wa karibu sana na Kiongozi Mkuu wa Chama na akionekana ana ushawishi sana wa kimaamuzi mbele ya Kiongozi Mkuu.
Selemani Msindi anatajwa kuwa kipenzi na chaguo mamba moja la Zitto Kabwe na kwa wanaofuatilia siasa za ACT Wazalendo wanaeleza kuwa anaweza kuwa Katibu mkuu mpya wa Chama hicho.
Ingawa Afande Sele hakubaliki kabisa na kundi linaloongozwa na Anna Mghwira kwa sababu za wazi kabisa, kuteuliwa kwake kuwa katibu Mkuu kutazidisha mvutano uliopo sasa na hatimaye kukiua kabisa chama hiki chenye tuhuma ya kutumiwa na CCM kwenye harakati zake.