Afadhali Rais Magufuli asieleweke

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Nimekuwa nikisikiliza hoja nyingi kwa wale wanaopinga hatua anazozichukua Rais Magufuli. Baadhi yao wanasema haeleweki. Wengine wanalalamika kuwa anavunja sheria. Lakini miaka yote hii tunafahamu kuwa Dk. Magufuli anaifahamu sheria tena vizuri kabaisa.

Lakini wapinzani wake hao wanashindwa kuelewa jambo moja kwamba, nyakati zimepita sana kwahiyo inahitajika nguvu ya mchakamchaka anayoifanya Dk. Magufuli ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu.

Lakini mimi nina mitazamo ya wazi kama Rais haeleweki ndio jambo zuri kwa kuwa wanasiasa wakimwelewa watamyumbisha. Naamini ili kukabiliana na watu wavivu, wazembe na watu ambao wao wanapenda kuamuriwa ndio wafanye kazi basi huyu ndio Rais amabaye ni dawa yao na kiboko yao.

Wanasiasa ambao wanajaribu kujipendekeza kwa Dk. Magufuli wameshindwa kupata mrejesho kama ambavyo walivyopata katika awamu zilizotangulia. Matokeo yake wameamua sasa kumkejeli Rais Magufuli kwa kudhani itamuumiza au kumfanya ashindwe kutimiza majukumu yake na kazi zake kwa wananchi.

Mwananchi yeyote anayetegemea na kufurahia kuwa Rais ashindwe kutimiza majukumu yake huyo atakuwa na matatizo. Baadhi yetu, tunaoamini katika mabadiliko ya kweli tuko nyuma ya Rais Dk. Magufuli kwa sababau tunaamini anaongoza na sio kutawala.

Kama mtawala angeweza kabisa kukubali mambo yaleyale akikubali kusukwasukwa na mawimbi ya maoni na mawazo ya kila namna kutoka kila kona. Lakini yeye kama kiongozi anajua anataka nini.

Tayari tunajua msimamo wake kuhusu kubana matumizi ya fedha za umma na madaraka. Tunajua maono yake kuhusu tatizo la msingi la nchi yetu- tunajua suluhisho lake amabalo alilipendekeza katika kampeni-“HAPA KAZI TU”.

Kuna wakati wa porojo na siasa za kuchangamsha genge. Chini ya Dk. Magufuli porojo na siasa za kuchangamsha genge havina nafasi na hazitakuwa na nafasi kamwe kwani sasa tunaelekea kwenye kujenga upya taifa letu.

Na inaonekana tunaanza kujenga kuanzia chini. Tunasimama nyuma ya Rais Dk Magufuli kwa sababu tunatambua kuwa jambo kubwa analolisimamaia limeelezwa vizuri kabisa na makamu rais Samia Suluhu Hassani kuwa kazi yao kubwa ni kuleta nidhamu- Na nidhamu inadsumbua.

Kuwataka watu wakae kwenye mstari mmoja mnyoofu wakati wamekishazoea kuchomoka chomoka na hasa kama kule kuchomoka kwenyewe kuliwafanya waishi mjini kiujanjaujanja.

Tunaunga mkono nidhamu hii kuanzia na matumizi ya fedha, matumizi ya muda, matumizi ya rasilimali zetu, nidhamu ya matumizi sahihi ya vipawa vyetu, ujuzi wetu na uwezo wetu.

Nidhamu hii kuirejesha na kuidumisha kunahitaji uongozi unaotambua kuwa- kama wanamuziki walivyoimba zamani-“nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio” ndiyo njia pekee ya kuweza kujenga taifa na jamii ya watu waliofanikiwa.

Tunatambua bila nidhamu ya kweli juhudi zote za kujiletea maendeleo zitakwama. Tunasimama nyuma ya Rais Magufuli kwa sababu tunaamini kuwa kwa wakati huu na zama hizi mpya Tanzania inamhitaji kiongozi amabaye siyo tu anajua anachotaka kufanya lakini anaonyesha pia namna ya kufanya mwenyewe.

Tunatambua pia kiongozi baada ya kusikiliza maoni na mapendekezo mwisho wa siku ni lazima aminki katika uwezo wake wa kusimamia anachotaka kufanya. Rais Dk. Magufuli mpaka sasa anafanya kazi nzuri na yenye kustahili pongezi kwa mara ya kwanza tunaweza kuona ni jinsi gani taifa lilivyokuwa limedekezwa na kuendekeza katika namana ya maisha kiasi kwamba ikawa starehe.

Starehe sasa imeisha watu wanatakiwa kuamka na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, taratibu na uongozi.

Kiongozi anatakiwa kuongoza na si kutawala. Dk. Magufuli sasa anaongoza. Tuko nyuma yake na tunamuunga mkono. Na binafsi naamini anaongoza kidemokrasia kufikia malengo yake ya kampeni. Tutafanya kila tunaloweza ili kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa wananchi nay ale yote aliyoyaahidi.

Wasiomwelewa Rais Dk. Magufuli ni wale waliozoea mfumo wa kuungaunga na kujipatia fedha haramu au zile zinazoatikanakwa njia ya mkato. Ni jambo muhimu kuelewa rais anachofanya kuhakikisha tunapata huduma. Tutahakikisha tunamuunga mkono ili atomize kila hatua ya malengo yake kwa nchi hii.

Hatuna sababu ya kuwaonea wale wote wanaomkosoa kwa kuwa wengine wanajisikia kufanya hivyo ili wasikilizwe naye. Lakini wanasahau kuwa hakuna rais duniani anayetekeleza kila anachoshauriwa na wanasiasa.

Bali Rais makini anatekeleza malengo yake na kuwashirikisaha wale wote wanaotakiwa kuyatekeleza. Kwa hiyo, mtu akija kumshauri kuwa atekeleze matakwa yake ni lazima ajifunze naye piakuwa naye kama rais ana malengo yake aliyoyapanga kuyatekeleza.

Ni wakati wa kuchapa kazi. ‘Ni wakati wa hapa kazi tu’.
 
Ukweli ni kwamba Magufuli anafanya mambo kwa papara hajii ashike kipi aache kipi kwasababu kila kitu nSadani ya mfumo kimeoza.
Sasa anataka kubadilisha mfumo huu ulioza na kujijenga zaidi ya miaka 50 kwa siku moja ni kitu ambacho hakiwezekani.
Naasipo pata washauri makini wakamsaidia akafanya mambo kwa utashi wake hii nchi itamshinda.
 
Mwambieni alivunje basi hilo jengo la makao makuu ya Tanesco hapo ubungo maji maana kwa sasa yeye ndo raisi, jk na pinda walomzuia kwa sasa wako chini yake
 
Magufuli watu wanamuelewa ndiyo maana wanampinga kwa vitendo vyake vya kukiuka haki za kidemokrasia kwa kisingizio cha maendeleo. Dunia nzima imethibitika nchi zenye democrasia ya kweli zimepiga hatua kubwa ya maendeleo
 
Ukweli ni kwamba Magufuli anafanya mambo kwa papara hajii ashike kipi aache kipi kwasababu kila kitu nSadani ya mfumo kimeoza.
Sasa anataka kubadilisha mfumo huu ulioza na kujijenga zaidi ya miaka 50 kwa siku moja ni kitu ambacho hakiwezekani.
Naasipo pata washauri makini wakamsaidia akafanya mambo kwa utashi wake hii nchi itamshinda.
Anayefanya mambo kwa papara ni Mbowe,

Alipokea mafisadi ili aende ikulu ,kiko wapi sasa.
 
Asante ujumbe mzuri sana , Magufuli Ni kiongozi wa kuigwa na kupewa sapoti Ni wapuuz tu ambao humpinga sababu amekuja na style mpya kabisa na anafanya yote kwa mujibu wa katiba iliyopo

Go Go Magufuli
 
Nyuma yake mnafuata nin?mtawala?kumbe mimi nilidhani ni kikngozi!!!!hata hivyo mbona ana kigugumizi kwa akina logomining?escrostanbit sandarous?ukiacha mengine?acheni unafiki maana Mungu ninayemjua mimi huwa hadhihakiwi hata mara moja
 
Unajenga hoja kwa kucompare na Mbowe, kwani mbowe Raisi? Na we ni ****"*""

Hoja ni utendaji wa presida jinsi anavyoapproach mambo na si kila kitu kukimbilia kumlinganisha na wapinzani.
 
Magufuli watu wanamuelewa ndiyo maana wanampinga kwa vitendo vyake vya kukiuka haki za kidemokrasia kwa kisingizio cha maendeleo. Dunia nzima imethibitika nchi zenye democrasia ya kweli zimepiga hatua kubwa ya maendeleo
Una uhakika?
 
ukweli ni kwamba magufuli ni jembe

naomba aendelee hivohivo tutanyooka tuu.
 
Anayefanya mambo kwa papara ni Mbowe,

Alipokea mafisadi ili aende ikulu ,kiko wapi sasa.

Hata kama hutaki kukubali time will tell.
Magufuli ni kama mpishi kwenye sherehe kubwa anatake yeye ndiye apike kila aina ya chakula kwa kuto hitaji wasaidizi. Huku tayari saa sita imeshafika watu saa nane wanataka wale chakula bado hajaivisha nusu ya idadi ya vyakula.
Sasa angali ametulisha wali mbichi kwenye bei elekezi ya sukari.
Sasa hiyo bajeti tutaiamini vipi wakati kwenye jambo moja amefeli je hhiyo bajeti iliyosheheni vitu kibao atatekeleza kwa ufasaha au ndio maamuzi yatachukuliwa kama ilivyo fanywa kwenye sukari.
Bahati nzuri tunaongea kwa mifano.
 
Magufuli watu wanamuelewa ndiyo maana wanampinga kwa vitendo vyake vya kukiuka haki za kidemokrasia kwa kisingizio cha maendeleo. Dunia nzima imethibitika nchi zenye democrasia ya kweli zimepiga hatua kubwa ya maendeleo
Na Dunia nzima mwangwi wa Dr Magufuri umetamalaki, naam sifa amejipatia. Labda kwa sababu Nabii hakubaliki kwao! Demokrasia mnayodai ina mipaka yake, na bahati mbaya hamjawahi kuwa nayo, zile zilikuwa fujo, na JK muunwana yule aliwaacha tu. Demokrasia inaiishia pale unapoingilia uhuru wa mwingine. Mwache RAIS afanye kazi tuliyomtuma, hacheni mazoea huu ni utawala mwingine
 
Back
Top Bottom