Afande Fojuman
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 657
- 548
Kuna rafiki yangu mmoja kanichekesha hadi machozi. Anasema siku zote ushindi wa ccm unachangiwa na wapiga Kura toka vijijini,lakini kwasasa upepo umebadilika. Anasema watu wengi vijijini watamchangua lowasa wakijua bado yupo ccm, yaani hawajui kuwa lowasa ameshahama. Anasema amejaribu kuprint picha Za lowasa na magufuri, lakini kila anayemuuliza atamchagua nani anamwonesha picha ya lowasa. Cha ajabu pia wengi wao hata magufuri hawamjui... Pia nywele nyeupe,ie mvi watu wengi uku vijijini wenye uelewa mdogo wanasema lowasa ni mtoto wa NYERERE. Hii, ni kama ya watindiga waliofikiri Nyerere anaishi baada miaka kadhaa kupita tangu kifo chake. Nimecheka sana)