Advance Bank na Mishahara Yao

Advance Bank na Mishahara Yao

MASTKEY

Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
9
Reaction score
3
Habari wana jf naomba mnifahamishe scale za mishahara ya client officer,client assistant na advisor.
 
mwaka juzi ilikuwa ni laki 2 kasoro mia mbili
 
wameniita kwenye interview kesho nasita kwenda mana mishahara kama ndo hivyo mmh majanga.
 
km umeitwa oral tegemea kukutana na directors wa kizungu
 
Mshahara unaweza kuwa mdogo ila mafanikio yakawa makubwa kutokana na akili yako inavyofanya kazi! usiogope mshahara!
 
Tengeneza cv acha kuangalia masilah kip bora kulala nyumban au kuchukua hyo lak kasoro!bt ukwel ni hvyo wanabana sana kwny masilah ya wafanyakaz bt icwe sababu ya wewe kuingia mitin!
 
Basic 450,000/= soon itakuwa 500,000/= monthly bonus up to half you salary,pia kuna annual bonuses reflective to ua performance,ukisign permanent contract unapata health insurance for your spouse and four dependants,ukifanya nao kazi kwa mwaka mmoja wanakupa life assurance ,etc CEO wa sasa ni mzuri hii bank ni nzuri,kama huna option kajaribu.
 
kama umechaguliwa katika timu ya Advance bank Tanzania, Jiandae kwa training ya miezi mitatu, na utakuwa ukipewa posho ya shilling 50,000 kila week kwa muda wote wa training, baada ya kumaliza vizuri training, utapewa mkataba wa miezi sita under probation,Kwa kipindi cha probation utakuwa unakula 500,000 na kama wataridhika na utendaji wako wa kazi kwa kipindi hicho cha miezi sita, watakuajili moja kwa moja na utakuwa unakula 600,000. Mshahara wa CA & TELLER ndio huo nilio kuonyesha, ila CO yeye anaongezewa kama 50,000 kwenye huo mshara niliouonesha. Pia Advance bank wanatoa bonas kutokana na utendaji kazi wako, ukiwa productive sana unaweza kujikuta kwamwezi unapata bonus nusu ya Mshahara wako. Kwa hiyo sasa kama umepata kazi hapo. Ninafikili Haka kakiasi kanaweza kukusaidia katika kusukuma ghurudumu la maisha na pia katika kukutengenezea CV yako. UAMUZI NI WAKO SASA KAKA, HIZO NDO UP DATE ZA ADVANS BANK TANZANIA. Pia kama unakwenda kufanya kazi mbeya, andaa nauli ya kukupeleka huko pamoja na fedha za makazi na maradhi, Kwa kipindi cha kwanza katika kazi utaona kazi chungu kama haukuwa na Maandlizi ya kutosha. kwani benk huwa haitoi fedha za usafili wala maradhi na Makazi, kwahiyo unaweza kuwa unatunza kiasi fulani cha fedha katika akiba yako ya posho kwa ajili ya Gharama za makazi na Maradhi utapokuwa umefika huko Jijini Mbeya.
 
Hakuna directors wa kizungu,wanaointerview ni mahr na matrainers waswahili tu..na english yao ni ya kawaida sana!mimi nimeshafanya oral!
 
Back
Top Bottom