Namshakende
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 771
- 1,904
Ndugu zangu Watanganyika,
Tunaumia. Taifa letu linapitia maumivu makubwa, na katika wakati huu wa majonzi lazima tukumbuke jambo moja muhimu: Machozi hayana dini. Waliouawa, walioteswa, waliopotezwa na waliopuuzwa hawakuulizwa kama ni Waislamu, Wakristo au watu wasiokuwa na imani. Wote walikuwa Watanganyika.
Dini hazijawahi kuwa chanzo cha maumivu yetu; chanzo ni chuki inayopandikizwa kwa maslahi ya wachache wenye tamaa. Ukatili na mauaji ya Mo 29 haya kuchagua imani , nasi pia hatupaswi kuruhusu dini zitugawe.
Leo, wapo wanaotafuta faida kwa kupandikiza sumu ya udini. Wana ndoto ya kuona Tanganyika ikipasuka vipande vipande ilhali wao wabaki salama kwenye viti vyao. Hao ndio hatari halisi ya taifa.
Lakini Watanganyika tumeamka, hasa kizazi kipya. Tunatambua kuwa adui yetu sio dini; adui yetu ni mifumo isiyowajibika, uongozi unaosahau watu, unaowateka watu, unaojificha nyuma ya pazia la Vyombo vya Ulinzi
Tunaona rushwa iliyokithiri ikigeuza mifumo ya serikali kuwa ni meza ya uporaji, ambapo rasilimali za umma zinahamishwa kwenda mifukoni mwa wachache. Tunaona dharau inayotawala, viongozi wakipuuzia vilio na maumivu ya wananchi. Tunashuhudia hofu ikimea, watu wakipotezwa, na utawala wa sheria ukikandamizwa. Rasilimali zetu zinauzwa kiholela kwa maslahi ya “Uzao” na walio madarakani, huku Mtanganyika wa kawaida akizidi kuzama kwenye shimo la umaskini.
Kwa wanaodhani wanaweza kutumia udini kutuficha mbali na ukweli wa rushwa, dharau na kupotezwa kwa watu, tunawakumbusha:
Nchi haianguki kwa njaa ya chakula; inaanguka kwa njaa ya haki.
Heshima ya kiongozi haitokani na ukubwa wa cheo, bali ukubwa wa kusikiliza sauti ya wananchi. Historia humhukumu anayetaka kugawa taifa, si anayeunganisha. Msicheze na moto ambao hamtaweza kuuuzima.
Tanganyika itasimama kama tutaungana katika maumivu haya , si kama maadui wa kidini, bali kama ndugu waliojeruhiwa na mfumo mmoja usiojali. Kila damu iliyomwagika ilikuwa ya Mtanganyika , si ya dhehebu.
Kwa hiyo, Sisi vijana tunasimama kwa sauti ya utu na kusema:
Acheni kutumia imani zetu kuficha ufisadi!
Acheni kupotosha kizazi kinachotafuta haki!
Tanganyika ni kubwa kuliko maslahi yenu.
Tuungane kudai Haki Kwanza.