Adui wa bara la Afrika

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
590
Reaction score
706
"Adui mpya wa Afrika si njaa, si vita, wala si ukoloni wa kiuchumi, bali ni kizazi cha vijana waliopata elimu kwenye memes, na hekima kwenye comments za Instagram! Hoja kwao ni mzigo, matusi ni talanta. Wakiona mjadala wanadhani ni fainali ya kurushiana maneno. Ujuaji wao mwingi kama mkia wa mbuzi, unatingisha tu, lakini hata mbu hawauogopi!" Alloyce, P.R.
 
Bora wao wa elimu ya memes kuliko hayo majizi yaliyosomeshwa bure alafu hayana faida zaido ya kuuza rasilimali za africa kama na wewe n .moja wa hayo majizi nikwamboe tu hivi tupo na NO REFORMS NO ELECTION
 
Ni kweli kabisa, kizazi cha sasa kimeporomoka kielimu na kimaadili. Mitandao ya kijamii imegeuka kuwa "chuo" cha vijana, wakijifunza kupitia mizaha badala ya vitabu. Wamekosa ustahimilivu wa kusikiliza hoja, badala yake hutumia matusi kama silaha ya kushinda mijadala. Hawana msingi wa maarifa. Kizazi hiki ni hatari kwa mustakabali wa Afrika iwapo hakitaelekezwa upya. Tunahitaji kurejesha misingi ya elimu, maadili, na fikra huru zenye tija ili kuokoa kizazi kilichopotea.
 
Maadui ni wale wanao generalize kila kitu kuhusu waafrika kwa kisa cha Insta.


Mnatambulika.
 
Tusiwasingizie vijana,leaders should play their part.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…