Adui ni Serikali na sio CCM.-Tupambane na serikali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adui ni Serikali na sio CCM.-Tupambane na serikali.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Sep 29, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Umoja ni nguvu ili kuing'oa CCM,

  Tatizo letu kubwa au labda niseme tatizo kubwa la vyama vya Upinzani katika juhudi za kuitoa Tanzania kwenye madhila inayoyakabili ni kwamba THEY ARE SO PREDICTABLE. Mara zote Vyama vya upinzani na nina maana ya mara zote tangu uchaguzi wa vyama vingi au mfumo to date ni kwamba wanafanya yale ambayo CCM na serikali zake wanawategemea wafanye. Wanazungumza maneno yale yale, wanafanya vitendo vile vile na wanakwenda kwa watu wale wale kutaka msaada na ushauri na zaidi wanawategemea watu au jumuia zile zile.

  Kwa hivyo imefika pahala leo CCM na serikali zake hata hawashughulishwi au kutishwa na Vyama vya upinzani tena. Upinzani umepoteza ile surprising factor yake. Umepoteza ule mvuto wake. Kwa maoni yangu inabidi Vyama vya upinzani vianze kufikiri nje ya box. Vinapaswa vijivumbue upya. In other words, must come with new strategies and they must approach CCM in a different way. They must use new tactics and strategies. They must look at CCM and its two government in a different way. Kwa kuanzia wasikubali tena upuuzi eti wapinzani wao ni CCM. CCM ni kundi la watu wachache wanaotafuta kila njia ya kujitajirisha wenyewe bila kujali maslahi ya wanachama wao na raia wote kwa ujumla. Hili ni jambo moja ambalo Upinzani wanaweza kulitumia na mifano iko mingi ya kuonyesha kwamba CCM hawana nia ya kuwaondoshea Watanzania kwa ujumla matatizo yanayo wakabili- hili suala la ufisadi ni mfano mmoja lakini kuna na mifano mingi mengine.

  Pili ni lazima waiambie dunia na Watanzania kwa ujumla kwamba mpizani wao ni SMT na SMZ na sio CCM. Kwani CCM ni kichaka tu wanachojifichia. Ukweli ni kwamba CCM wanatumia vyombo vya serikali kufanikisha malengo yao. Hili ni jambo ambalo linaweza kupelekwa hata mahakamani ili ionyeshwe ni vipi SMT/SMZ zimekuwa ni matawi ya CCM. Mfano ni kwamba polisi, JWTZ, usalama, ofisi ya rais wote wa ZNZ na TZ zinatumika kuendeleza maslahi ya CCM.

  Tatu tume zote za uchaguzi sio huru. Zimeundwa kwa kutumia wanachama au wapenzi wa CCM. Kwa nini Wapinzani wasidai kwamba tume hizo ama ziundwe kwa kuwa na wajumbe sawa kutoka kila chama au wajumbe wake wasiwe wanachama au wapenzi wa chama chochote. Na zaidi kwa nini wasidai kwamba wajumbe wa tume ya uchaguzi wasiwe wanajibu kwa rais yoyote yule. Iwe mathalan wanawajibika kwa baraza la wawakilishi na bunge? Bora zaidi kwa nini wasidai muundo wa tume ya uchaguzi uwe kama vile ilivyo fanywa Afaghanistan i.e. tume yenyewe wajumbe wake ni WaTZ lakini juu yake kuna Tume ya rufaa ya uchaguzi ambayo inaundwa na wajumbe kutoka nje ya TZ, mfano EU, UN, Commonwealth n.k.

  Upinzani unatakiwa uhakikishe kwamba kila inalolifanya/kusema inaweza kulitekeleza. Wasiwe kama CCM kutoa ahadi ambazo hawawezi kuzitekeleza. Ni lazima matendo yao na kauli zao zionyeshe tafauti ya wazi baina yao na CCM. Kwani hivi sasa hakuna tafauti yoyote. Pia wakubali kukoselewa na wapokee maoni ya wengine. Ni muhimu sana kwa manufaa ya Tanzania na WaTanzania wote kwamba wawakilishi/wabunge ambao lengo lao ni kujinufaisha wao binafsi waachwe na iwe ni kawaida kwa wabunge/wawakilishi wa upinzani kukutana na raia wa majimbo yao ya uchaguzi bila kujali wanatoka chama gani. Wawe na siku maalum na ofisi maalum katika majimbo yao ambapo wanakutana na raia kusikiliza matazo yao na shida zao. Isiwe biashara ya kuonana kila unapofika uchaguzi au wanapopita na magari yao makubwa huku wakiwarushia mavumbi wale walio wachagua.

  Ama kuhusu suala la muungano na Zanzibar, ninadhani kwamba wajumbe wa ukumbi huu na hata wasio wajumbe, as long as we share same beliefs and principles, tunaweza kulipeleka suala hili kwenye vyombo vya kimataifa kutaka ufumbuzi na zaidi kuudadisi uhalali wa Muungano. Kwani the so called Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio muungano wa ridhaa, at least hivi sasa ridhaa haipo tena, yaliyobakia ni mabavu tu. Huu sasa ni ukoloni na sisi kama WaTanzania hatuna budi kuupinga.Kwa kutumia vyama vyetu vya upinzani ,sio tunaburuzwa na itikadi za kiCCM.

  Naomba kuwasilisha hoja ukumbi wa JF.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  serikali ni ya ccm sasa unasemaje adui yetu ni serikali na sio ccm?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni sawa kabisa ,ila ufahamu kuwa unapombana Waziri au Raisi sidhani kama unaibana CCM.
  Unapoishitaki serikali sidhani kama unaishitaki CCM.
  Vyombo vya serikali(Dola) havitakiwi kuamrishwa na kufuata matakwa ya CCM ,vinatakiwa kufuata sheria za Nchi na hivyo hivyo serikali iliyokuwepo madarakani haitakiwi kufuata katiba na sheria za Chama chake inatakiwa kufuata Katiba na sheria za nchi ya Nchi.
  Serikali iliyokuwepo madarakani inawajibika kwa wananchi wote bila ya kutazama huyu anatoka chama gani, kwa lolote lile iwe wakati wa shida au raha.
  Serikali inatakiwa iwe kwenye utawala au utaratibu mwengine kabisa na sio wa itikadi za Chama,zipo sheria za nchi hapo ndipo inapobanwa serikali.
  Serikali hailaumiwi kwa jambo jingine zaidi ya kuvunja na kuvuruga sheria za nchi.
  Tume ya Uchaguzi si ya CCM inakuwaje inaundwa na CCM watupu ,Tume ni chombo cha serikali kisichofungamana na chama chochote kile cha siasa kama inavyotakiwa kwa msajili wa vyama.
  Natumai tunaweza kuitenga serikali na kuibebesha lawama ,tuna mafisadi kibao wametujalia ,kinachotakiwa sio tuisakame CCM,ikiwa mafisadi wanapeta wakupigwa dongo ni Serikali na sio CCM,kwa maana ingine serikali haifuaati sheria za nchi ,inaweza kuwajibishwa kwa nguvu za wananchi walioelimishwa kikamilifu na kuelewa umuhimu na stahili au wajibu wa serikali.
  Natumai utakuwa umepata picha. Ulimsikia Kikwete UN juzi aliposema kuwa Serikali haihusiki ni mambo ya kichama ,akimaanisha kujitenga na kuitenga serikali na mambo ya kichama ,hapo ndipo anapotakiwa au inapotakiwa hata kule kwenye TUME kuwepo huru kusiwepo na harufu ya UCCM.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukisikia kuchanganyikiwa ndio huku sasa
   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mr Masatu,
  Usichanganyikiwe mkuu hayo ni mambo harisi katka Serikali yetu na CCM kinachofanyika huku ndicho hufanyika kule i mean Serikali na CCM, tulia na uwasomee ramani Usiwashtukia kwa sasa we waache watakuja shangaaa siku yakiwatokea puanai.

  Wana JF me nilitaka tu kutoa mfano mmoja nao huu ndio nao ufahamu ulitokea kwa alieyekuwa PM EL, alibahatika kukutana na binti mmoja nae ni mkuu ya wilaya fulani kwa sasa ana msimamo usipime, EL alimwamisha aliko kuwepo na kuja Monduli ila alipambana na vingozi wa CCM ktika halimashauri ya wilaya hio na wakaenda kumsemea kwa EL kuwa hakisaidii chma kwashughuli zitendazo na CCM jamani tena kwakutaka kutumia magari ya serikali, yani viongozi wa CCM monduli wamejisahau sana.EL alipo kuja kumhoji mkuu wa wilaya ambae yeye mwenye EL alifanya mpango aje pale Monduli ili kuimalisha maendeleo ya wilaya ile kwani alikoto alikuwa akichapa kazi ipasavyo.Mwishowe mkuu huyo wa wilaya alia hamishwa kwenda kwingine nako maendeleo yako poa. Sasa hapo ndipo mtajua kuwa kunaviongozi wengine ni makini sana na viongozi wengine wapo pale kwa manufaaa yao wenyewe na watu furani katika koo zao,

  Basi Nchi irudishwe katika majimbo tuone tutavyo wakamatia kati hao watakao jitia ndio viongozi kwa Ukiwa kiongozi ktk majimbo utawajibishwa mapema sana bila kuchereweshwa na kujiuzuru juuu
   
Loading...