Adui namba moja ya watanzania ni eliaza feleshi - Director of public prosecution

bona

JF-Expert Member
Nov 6, 2009
3,798
1,435
wana JF leo tumjadili director of public prosecution ndugu eliaza feleshi, wengi wetu tunailaumu pccb kua haiwachunguzi wala rushwa na mafisadi lakini kazi ya pccb wakishamaliza file lote wanampelekea huyu bwana yeye ndo awafikishe mahakamani kwa hiyo mapambano ya ufisadi ktk tanzania hayatafanikiwa bila huyu bwana kua shupavu, yeye kila file analopelekewa anadai ushahidi haujitoshelezi kwa hiyo hawezi mburuza huyo mtuhumiwa mahakamani eti serikali inaweza shindwa kesi na kudaiwa fidia kubwa ambayo ikilipwa italeta hasara kwa serikali, swali la kujiuliza hadi pccb wampelekee file si kua wamejiridhisha kuna kesi ya huyo mtu kujibu kwani hata pccb wana kitengo cha sheria!
 
Mtu akishakuwa mteule wa Rais unategemea nini Mkuu?
Ishu zote za Grand corruption kwa namna moja ama nyingine zina mahusiano na wakulu, sasa ni lazima awa'consult kabla ya kuproceed na matakwa ya sheria!
 
na mbaya zaidi hii post ni ya kuteuliwa na rais, mifumo ya sheria ya nchi hii imebuniwa kuwalinda watu wa jamii fulani suala la sheria msumeno halipo! cha kusikitisha huyu bwana ana power hata ya kumsamehe mtu asishtakiwe pasipo yeye kuhojiwa na yoyote! ana declare tu state does not wish to proceed with a case against mr.X thats it!
 
ofisi badala ya kujaa vitendea kazi imejaa mafile ya takukuru mpaka darini
 
Sasa kumbe unajua kua DPP ni mteule wa yule jamaa?
Kama ndivyo basi ilitakiwa useme kua yule jamaa ndio adui yetu mkubwa
 
Kutokana na mgongano huu wa kimaslah pamoja na kulindana, ndio maana wadau wanapendekeza tuwe na muendesha mashtaka wa UMMA
 
kiasili watanzania tuna maadui watatu na si mmoja. Ni ujinga, umasikini na maradhi. Feleshi hawezi kuwa adui yetu bali huyu ni mwathirika wa ufisadi
 
Mimi kwangu adui namba 1 ni taasisi ya urais, ambayo feleshi yupo chini ya hyo taasisi.
 
katiba mpya ndio dawa; tenganisha urais katika uteuzi wake; ateuliwe na bunge
 
nilileta hii thread hapa at least wajue kua kuna vikwazo vingi sana ili mapambano ya ufisadi yafanikiwe! this guy has got the easiets job fo all public servant, he doesnt even get media attention!
 
Back
Top Bottom