MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Adui Mkuu wa CCM Zanzibar siyo CUF bali ni Muungano. CUF wanatumika tu kama gari lililobeba manung’uniko waliyoaminishwa sana Wazanzibari wengi.
Makosa ya CCM Zanzibar ni kuwaaminisha sana Wazanzibari kama Muungano ‘’unawanyonya’’ halafu wanashindwa kutimiza ahadi walizowaahidi za kuondoa ‘’unyonyaji’’ waliodai unalindwa na serikali mbili. Takwimu za maoni ya Wazanzibari kwenye tume ya Jaji Warioba zilionyesha kwa upande wa Zanzibar, asilimia 60 walipendekeza Muungano wa Mkataba.
Kwa wale wanazifahamu vizuri siasa za Zanzibar wanafahamu matatizo kuhusu Muungano yameanza kabla ya kuungana rasmi lakini kilele chake kilikuwa mwaka 1982.
Mwaka 1984 tulishuhudia Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na Makamo wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aboud Jumbe Mwinyi, alilazimishwa kujiuzulu katika Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma akishutumiwa kutaka kuvunja Muungano.
CCM Zanzibar waliwaahidi Wazanzibari kuwaletea serikali tatu kama mwarobaini wa ‘’unyonyaji’’katika kikao cha Bunge Maalum la Katiba lakini walipofika Dodoma wakabadilika na kuwa ndumila kuwili na kigeugeu kinyume na makubaliano yao wakati wakiwa Zanzibar.
Tulishuhudia pale Dodoma wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar wakishutumiana na kulaumiana wao kwa wao kwa kusaliti makubaliano yao ya kushinikiza serikali tatu kabla hawajafika Dodoma. CUF wakasimama kwenye makubaliano yao na matokeo yake, CCM Zanzibar kwa sasa wanaadhibiwa na Wazanzibari wengi kwa kukiuka makubaliano yao!
Sio kwamba Wazanzibari wengi wanamuona Maalim Seif kama kiongozi mwenye maono na Madhubuti, la hasha. Maalim Seif kwa macho ya Wazanzibari wengi ni kimbilio la mwisho(last resort) katika kudai na kupigania kurejesha Mamlaka Kamili ya Zanzibar kupitia serikali tatu ambayo wameaminishwa sana na baadhi ya viongozi wa CCM na CUF. Maalim Seif anautumia udhaifu wa viongozi wa CCM katika misimamo madhubuti kama mtaji wa kisiasa. Hata Maalim Seif anafahamu vizuri mamlaka kamili ya Zanzibar hayawezekani katika serikali tatu.
CCM Zanzibar wanapoteza muda kukimbizana na CUF wakati adui wao ni CCM wenyewe ambao wamewaaminisha sana Wazanzibari kuwa Muungano wa serikali mbili ni kama ‘’mkoloni mweusi’’ kutoka Tanzania Bara. CCM Zanzibar kwa sasa wanajikaanga kwa ahadi zao kuhusu Muungano.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, “Uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi. Hoja za Muungano kwa upande wa Zanzibar ambazo zimeshindwa kusimamiwa ipasavyo na viongozi wa CCM kwa sasa zinakaribisha mainzi na mafisi!
Vikundi kama vya UAMSHO ni zao la hoja za Muungano. Kuna vikundi vingine vinadhani Muungano umezuia Zanzibar kuwa officially nchi ya kiislam na kwa misingi hiyo, vimejiegemeza kwenye CUF ili kutimiza ndoto zao za kuiona Zanzibar ni nchi ya Kiislam.
Mpaka pale viongozi wa CCM watakapo kuwa wakweli katika nafsi zao na kiutendaji, CUF itaendelea kushamili kama gari lililobeba manung’uniko waliyoaminishwa Wazanzibari wengi katika ndoto ya mamlaka kamili ya Zanzibar.