Adui mkubwa wa maendeleo ya mwanaume ni mwanamke!!

Adui mkubwa wa maendeleo ya mwanaume ni mwanamke!!

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
2,617
Reaction score
2,267
Salaam wakuu? Maisha magumu si utani na kwa wale wenye afueni Mshukuruni Mungu kwa sana msikufuru.

Nimekuwa nikifikiria sana ni kwanini sisi wanaume hasa vijana kupata maendeleo ya kiuchumi ni ngumu sana wakati tuna akili, afya njema na nguvu za kutosha kutafutia mali!?

Achana na hoja ya uvivu, tuzungumzie wale wanaojitumikisha kwa sana na wenye kipato lakini maendeleo kwao hayaonekani, kwanini? Nionavyo mimi mwanamke anawezakuwa tatizo namba 1. Imezoeleka kwa familia nyingi za kiafrika mwanamke huanza kutafuta mali baada ya kuwa na mwanaume (bwana) ila mwanaume huanza kutafuta mali kabla yakuwa na mwanamke(bibi).

Mbaya zaidi ni hata pale ambapo mwanamke ana kipato kikubwa kumzidi bwana wake bado atahitaji kumtegemea bwana huyo kwa kila kitu, yaani cha mwanaume ni chawote ila cha mwanamke ni chake peke yake. Na kadri mwanaume anapojitahidi kutafuta ndivyo mwanamke anavyoongeza matumizi.

Katika mazingira kama haya ndio nimebaini adui mkubwa wa maendeleo ya mwanaume ni mwanamke.
 
Kwa kijana miaka 20's kwenye mahusiano kwa haraka haraka hadi ale mzigo hawezi kuepuka kuumizwa kuanzia 50k.

Sasa hapa sijaweka kwa mwaka itakuwaje.
Ila mkuu inategemea haya mambo hayana kanuni kuna watu wanapambana na mwanamke amewekwa mbali ila hali bado ni mbaya.
 
Maelezo yake yanaashiria kuwa huna uzoefu wa kutosha wa kuishi na binadamu hawa wa jinsia ya ke. Umerahisisha mno hitimisho lako, lakini nikwambie tu kwamba wanawake hubadilikabadilika katika mahusiano, kuna wakati ni wazuri,wema, wafariji, wenye upendo na kila kila sifa nzuri unayoweza kuongeza hapo! Ni wakati huo ambapo ambapo utajivunia mwenza na kumshirikisha siri zako ili kupunguza kubeba mambo mengi kifuani mwako...

Hata hivyo, hali hiyo si ya kudumu kamwe, hufikia kipindi wenza wetu hawa hubadilika kabisa kwa sababu zisizoelezeka kirahisi tu, wakati huu unaweza kuwaita kila jina baya na bado usiwapatie... Ni kipindi cha majuto makubwa kwa mwanaume, usipokuwa makini kisaikolojia unatoka relini na kuathiri uzalishaji na miundombinu yako.

Mpende mkeo kwa tahadhari, she is not your mum..

Pamoja na udhaifu wao, bado tunawahitaji, kuna kizuri ndani yao ambacho hutufanya kuwahitaji iwe kwa kuhonga, kuwarubuni ama kuwapenda kwa dhati. Si rahisi kufanya hayo kwa adui yako, hivyo wanawake si adui kabisa.
 
Let me be the last person to say this

Kama huna akili, USIOE

Thank me later
 
Siku ukijua kutofautisha kati ya mwanamke na MKE nitafute kwenye namba yangu ya voda.
 
Inategemea umeoa mke wa aina ipi, kuna wengine wanapambana na wanaweka chakula mezani na mnaenda bega kwa bega Lkn ukichukua hawa kuku wa kisasa utajuta.
 
Maelezo yake yanaashiria kuwa huna uzoefu wa kutosha wa kuishi na binadamu hawa wa jinsia ya ke. Umerahisisha mno hitimisho lako, lakini nikwambie tu kwamba wanawake hubadilikabadilika katika mahusiano, kuna wakati ni wazuri,wema, wafariji, wenye upendo na kila kila sifa nzuri unayoweza kuongeza hapo! Ni wakati huo ambapo ambapo utajivunia mwenza na kumshirikisha siri zako ili kupunguza kubeba mambo mengi kifuani mwako...

Hata hivyo, hali hiyo si ya kudumu kamwe, hufikia kipindi wenza wetu hawa hubadilika kabisa kwa sababu zisizoelezeka kirahisi tu, wakati huu unaweza kuwaita kila jina baya na bado usiwapatie... Ni kipindi cha majuto makubwa kwa mwanaume, usipokuwa makini kisaikolojia unatoka relini na kuathiri uzalishaji na miundombinu yako.

Mpende mkeo kwa tahadhari, she is not your mum..

Pamoja na udhaifu wao, bado tunawahitaji, kuna kizuri ndani yao ambacho hutufanya kuwahitaji iwe kwa kuhonga, kuwarubuni ama kuwapenda kwa dhati. Si rahisi kufanya hayo kwa adui yako, hivyo wanawake si adui kabisa.
Asante mkuu, ila neno Adui labda nimelitumia kimakosa pengine ningesema kikwazo au hata changamoto ungenielewa vyema nilichomaanisha.
 
Siku ukijua kutofautisha kati ya mwanamke na MKE nitafute kwenye namba yangu ya voda.
Sawa mkuu, ila kumbuka kuna watu wanaishi pamoja na wanafamilia lakini hawajaoana, watu kama hao sidhani kama wanatofauti na wanandoa
 
Back
Top Bottom