Adidas wana mkono wao katika tuzo ya Messi?

Adidas wana mkono wao katika tuzo ya Messi?

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
Lionel Messi ndie mchezaji bora wa Kombe la Dunia 2014 kufuatia kutajwa baada ya michuano hiyo kuisha juzi Jumapili na Ujerumani kuibuka washindi kwa kuwafunga Argentina.

Kupewa kwake tuzo hiyo kukapokelewa kwa mitazamo tofauti, wapo waliounga mkono na wapo walioponda hatua hiyo wakidai ni upendeleo wa wazi kwa staa huyo wa Argentina.

Wapo waliokuja na maneno mepesi, lakini walionigusa ni waliokuja na hoja nzito kuhusu ubora wa Messi wakimlinganisha na wachezaji wengine kama Manuel Neuer, Arjen Robben, Thomas Mueller na James Rodriguez.

Kwanini nimewataja Adidas kwenye kichwa changu cha habari? Kampuni hii ya vifaa vya michezo ndio wadhamini wa Messi, na zaidi ni washirika rasmi wa FIFA kwa miaka kadhaa sasa. Walioponda uteuzi wa Messi kuchukua tuzo walikuja na hoja nzito kuwa huenda FIFA wamefanya hivyo kwa sababu za masoko, yaani kutoa tuzo kwa mtu ambaye atakuwa na faida kwao kibiashara.

James, Muller, Neuer na wengineo si maarufu kama alivyo Messi. Si mara ya kwanza FIFA kukiuka mambo ya kimchezo kwa sababu za kibiashara. Sakata la kupimwa afya kwa wachezaji wa Costa Rica na madai ya kupendelewa waziwazi kwa baadhi ya timu 'kubwa' kunakuja pamoja na tuhuma hizi. Zote zikihusishwa na makampuni makubwa kupata hasara ndapo timu pendwa zitaaga mashindano mapema.

Adidas ni mabepari na wanataka faida zaidi, kama wakipata fursa ya kushinikiza nani awe mchezaji bora sidhani kama wataacha kumpendekeza aliye upande wao. Ushawishi wa Adidas juu ya FIFA sio wa kuhoji, mipira yote maarufu inayochzewa Kombe la Dunia ni kazi ya mikono yao, achilia mbali jezi na vifaa vyote vya waamuzi, waokota mipira na yeyote anayehusika katika michuano hii.

Kwa mara ya kwanza utaratibu uliozoeleka wa kuchagua mchezaji bora ulikiukwa. Badala ya jopo la waandishi wa habari kuchagua, kamati maalumu ndio iliamua tuzo za michuano hii.

Kituko kingine kikajiri baada ya tuzo, kiongozi mkuu wa FIFA akadai 'eti' ameshtushwa na uteuzi huo. Ndio, Sepp Blatter nae hakutarajia kuwa Messi angepewa tuzo.

Ni rahisi kuhisi haya ni maigizo, kwani sio kweli kwa kinara huyo wa FIFA kutokuwa na fununu kuhusu taarifa nyeti kama hiyo. Kukanusha pengine ilikuwa ni janja ya kuhamisha umakini, wada weseme 'Si unaona, hata Rais alikuwa hafahamu!'

Haya ni mawazo mbadala tu.

CC: AshaDii

2405222_full-lnd.jpg
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom