TANZANNIA
JF-Expert Member
- Sep 29, 2015
- 1,047
- 385
Nimeshangazwa sana na adhabu walizotoa TFF kwa timu zilizopanga matokeo na baadhi ya wahusika.
Si kwamba naunga mkono madudu yaliyofanywa na timu hizo au watu hao bali ni aina ya adhabu walizotoa, unamfungia mtu maisha wakati ajira yake ni mpira, adhbu hii inastahili? unamfungia mchezaji miaka kumi na kumtoza faini ya milioni,10/-ukiangalia huyo mtu tayari ana umri wa miaka 26 unapomfungia miaka kumi atakuwa na umri gani? unamtoza faini ya milioni kumi wakati mshahara wake/kipato chake hakifiki hata laki tano kwa mwezi!
Tuangalie anga za kimataifa wakati Suarez wa Uruguay alipoikosesha Ghana kwa makusudi kwenda nusu fainali ya kombe la dunia 2010 South Africa kwa kudaka mpira uliokuwa unaingia wavuni alipewa adhabu ya kufungiwa mechi tisa tu za timu ya taifa.
Pia Zidane Zizu aliwahi kumpiga mtu kichwa uwanjani lakini alipewa adhabu ya red card na faini kama sijakosea, na si kumfungia mtu maisha kwani huko ni sawa na kumuua kwani ndio ajira yake.