Adhabu ya Chirwa yanukia Usimba

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Utamfungia vipi mchezaji tegemeo wa timu kwa muda usiojulikana? Ameua mtu? Hii ni hujuma kwa Yanga sawa na hujuma nyingine kwenye mpira.
 
Wamlipe hela yake sio kumfungia yani clubs za bongo hazina tofauti na serikali ya pombe wanakudhurumu ukilalamika wanakuadhibu
 
Si kweli, deni halipungui kwa kumfungia mchezaji kwa muda usiojulikana, mwisho wa siku mtamlipa tu bila kufanyakazi.
 
Utamfungia vipi mchezaji tegemeo wa timu kwa muda usiojulikana? Ameua mtu? Hii ni hujuma kwa Yanga sawa na hujuma nyingine kwenye mpira.
Mimi sioni tatizo mchezaji kufungiwa pale anapobinika kufanya makosa. Mambo mawili ndiyo yananipa ukakasi kwenye huu utaratibu wa kutoa adhabu: 1. Adhabu kutolewa muda mrefu baada ya kosa kufanyika. Kuna tatizo gani kuandaliwa utaratibu utaopitia Ripoti ya Mwamuzi mara tu baada ya mechi kukamilika na adhabu kutolewa kabla ya mechi inayofuata? Kwa sababu mchezaji aliyekosa ni haki yake kuadhibiwa. Na timu iliyokosewa na mchezaji huyo ni haki yake kuona mchezaji huyo anaadhibiwa. Kadhalika na mwamuzi. Na wanasema kuchelewesha haki ni kunyima haki. Sasa mchezaji anapofungiwa miezi kadhaa baada ya kosa, wakati tayari ameshacheza mechi kadhaa tangu mechi hiyo kufanyika ndiyo ameadhibika ipasavyo? Jaalia ndani ya mechi hizo alikwishaipatia ubingwa timu yake (au ilikwishashuka daraja au ilikwishapata uhakika wa kunusurika kushuka daraja), adhabu hiyo itakuwa imesaidia nini? Si ni kama kumsomea hukumu maiti kaburini? 2. Kumwadhibu mchezaji mara mbili. Kwanza kwa kumsitisha kucheza na baadaye kuitaka Kamati ya Ligi kumhukumu. Kwani hiyo Kamati haiwezi kufanya kazi yake bila ya kuamriwa?
Mambo mawili hayo yasiporekebishwa lazima sura ya upendeleo kwa na chuki dhidi ya timu moja ama nyengine itajitokeza.
 
Tff hii ni mbovu kuliko zote. Adhabu lazima itolewe haraka baada ya tukio na izingatie kutunza kipaji cha mchezaji. Kumfungia mchezaji kwa muda usiojulikana ni hujuma kwa mchezaji na club yake.
 
Utamfungia vipi mchezaji tegemeo wa timu kwa muda usiojulikana? Ameua mtu? Hii ni hujuma kwa Yanga sawa na hujuma nyingine kwenye mpira.
Soma sheria za soka uelewe. Adhabu haina kuangalia mchezaji tegemeo, embu angalia mwanandinga ghari Neymar wa PSG alikuwa kibano pia kwa utovu wa nidhamu aisee
 
Alifungiwa kwa muda usiojulikana? Mchezaji apigwe faini au aambiwe anasimamishwa kwa mechi ngapi kama adhabu ya kosa lake. Sio kutoa adhabu ya kiiiihun baada ya muda mreeefu kosa kutendeka.
 
Emanueli Okwi naye anafaa kufungiwa kwa muda mrefu hapo Simba sc.
Hiki kijamaa kinaringa sana pindi kikisajiriwa na timu zetu za hapa mjini.
Mfungieni Okwi anakula mshahala wa bure bila kufanya kazi
 
Utamfungia vipi mchezaji tegemeo wa timu kwa muda usiojulikana? Ameua mtu? Hii ni hujuma kwa Yanga sawa na hujuma nyingine kwenye mpira.
Sijaelewa kitu, huyu Chura kafungiwa Nini? Acheni aendelee kulima mahindi na matikiti huko Zambia bhana, kama mshahara wenyewe ndio wakusotea hivyo si bora apambane na Hali yake!
 
soka la bongo, watazamaji tunaona aibu ila viongozi walaa ndo kwanza wanatuna na kujiona wao ndio kila kitu.
 
Back
Top Bottom