ADF yashambulia majeshi ya UN

ADF yashambulia majeshi ya UN

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,321
32D09D2E-9E99-45B7-B94A-FDF40CB68CC3_w1023_r1_s.jpg

Wapiganaji wa Uganda wamefanya mashambulizi katika kambi ya kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Shambulizi hilo limemuuwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (UN) na kujeruhi dazeni ya watu, kwa mujibu wa tamko la majeshi ya UN, MONUSCO, na jeshi la Congo.

Msemaji wa Jeshi la Congo Mak Hazukay amesema kuwa anaamini waasi wa kikundi cha Allied Democratic Forces au ADF kikundi cha wapiganaji wa Kiislam wa Uganda, kilihusika na shambulizi hilo, na pia mapambano mengine katika eneo hilo katika siku za karibuni.

Kituo cha kijeshi kilichoko karibu na mashariki ya mji wa Beni pia kilishambuliwa mapema Jumatatu.

Uraia wa wale waliouawa na kujeruhiwa katika shambulizi hilo haukufahamika mara moja.

Chanzo: Voa swahili
 
ADF au ALLIED DEMOCRATIC FORCES halafu eti ni wapiganaji wa kiislamu lakini hatukusikia wale LORD RESISTANCE ARMY wakiitwa wapiganaji wa kikristo. Karne hii waislamu na hii fitna inayoendelezwa si ya kawaida. Menyezi Mungu atatupitisha salama.
 
Mkuu usiwe hivyo...wale was lords resistance army walikuwa wanatajwa kabisa kuwa wanataka kutawala Uganda kwa kutumia amri kumi. Labda kipindi kile mitandao haikuwa imezagaa kama leo lakini nakumbuka hivyo ndivyo walivyokuwa wanaatajwa. Tena Koni alikuwa anaitwa prophet kabisaa.
Shida ni kwamba kwa upande wa hawa wanaoitwa wapiganaji wenye mlengo wa imani ya kiislam labda wamekuwa wengi au taarifa zinapatikana kwa ukaribu zaidi
 
Nisiwe hivyo niwe vipi? Mnalishwa maneno na vyombo vya magharibi na njaa zeninayabeba mazima mazima.
 
Mkuu mbona wanatajwa sana hata wale central African republic wanatajwa
 
VOA wameripoti kifo kimoja na majeruhi 15 wahanga ni majeshi kutoka Tanzania.
Kitu nisicho kielewa ni kuwa hawa waasi ni wa Uganda yahani wanapinga Museveni na serekali yake. Sasa inakuwaje waishambulie Congo na kuuwa wakongo? . Huu siyo uhuni wa Museveni kweli?? Ilitarajia hujuma zao zielekezwe Uganda!
 
aisee upo akilini mwangu inakuwaje washambulie kongo wakati
 
ADF au ALLIED DEMOCRATIC FORCES halafu eti ni wapiganaji wa kiislamu lakini hatukusikia wale LORD RESISTANCE ARMY wakiitwa wapiganaji wa kikristo. Karne hii waislamu na hii fitna inayoendelezwa si ya kawaida. Menyezi Mungu atatupitisha salama.
uislam hustawi katika mazingira ya shida na kusongwa..ndio dini inayokua kwa kasi kuliko zote chini ya jua
 
Back
Top Bottom