ADC yajitosa Bububu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ADC yajitosa Bububu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  NA MWANDISHI WETU

  29th August 2012

  [​IMG]

  Mwenyekiti wa muda wa chama cha siasa chenye usajili wa kudumu cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraaj Abdallah (kushoto), akipokea cheti cha usajili wa kudumu wa chama chake kutoka kwa Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, Rajabu Juma, kwenye hafla iliyofanyika katika ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam jana.  Chama cha Aliance for Democratic Change (ADC) kimesema kitashiriki katika uchaguzi mdogo wa wawakilishi katika jimbo la Bububu visiwani Zanzibar Septemba 16, mwaka huu na hivyo kufanya idadi ya vyama tisa vitakavowania nafasi hiyo.

  Akizungumza baada ya kupewa usajili wa kudumu, Mwenyekiti wa ADC Taifa, Said Miraji, alisema kwa sasa chama chake kimeweza kupata wanachama 200 kila mkoa katika mikoa 10 hivyo kinaweza kushiriki uchaguzi wowote nchini.

  Alisema kwa sasa wanafanya uchaguzi ndani ya chama kumpata mgombea wa nafasi ya uwakilishi katika jimbo la Bububu visiwani Zanzibar.

  "Tutafanya uchaguzi wa kwanza ambao tutampitisha mgombea Urais pamoja na mgombea katika uchaguzi jimbo la Bububu," alisema Miraji.

  Miraji alisema chama chake kitaendesha kampeni za kistarabu pasipo vurugu, na kukemea vitendo vya ubaguzi wa dini na ukabila.

  Naye Naibu Msajili Mkuu wa vyama vya siasa nchini, Rajab Juma, aliwapongeza ADC kwa jitihada kubwa walizozifanya hadi kupata usajili huo na kusema wazingatie masharti waliyopewa vinginevyo watanyang'anywa usajili huo.

  Alisema, katika mikoa waliyozunguka, waliweza kuthibitisha wanachama hai ambao ni Mwanza (203), Kusini Pemba (233), Mjini Mngharibi (290), Tabora (273), Dar es Salaam (291), Dodoma (305), Mtwara (203), Lindi (246), Mara (253), na Tanga (291).

  Kusajiliwa kwa ADC na kunaifanya Tanzania iwe na vyama 20 vyenye usajili wa kudumu.


  CHANZO: NIPASHE


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hiki Ni Chama kama CUF kimazingira?
   
 3. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  naona pro cdm mshaanza kuogopa ehh!...
   
 4. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,587
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  bora hata cuf!
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  lol...
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  I wish I was Pro Chadema
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,740
  Trophy Points: 280
  Yule mwanasheria wao aliye kuwa anatoa povu jana sijui kapotelea wapi?

  Hongera sana ADC
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  nilidhani weye ni pro cdm! sababu wao hulka yao ni uwoga na umimi wa kutaka kuwa peke yao wawe ndio chama cha upinzani .. mfano umimi wanaofanya bungeni kutenga vyama vyengine vya upinzani
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,740
  Trophy Points: 280
  Njiwa nao siku hizi hawafugiki!
   
 10. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  ndio vizuri
   
 11. m

  majebere JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Acha waongezeke kuzigawa kura.
   
Loading...