Ada juu Chuo Kikuu Tumaini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ada juu Chuo Kikuu Tumaini.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mmaroroi, Jul 23, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chuo Kikuu Tumaini kimepandisha ada kutoka 1,500,000/= hadi 2,500,000/=.Hii haitakuwa pigo kwa walalahoi? na nini maana kwa Serikali kuondoa kodi kwa taasisi za dini?
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  What triggered this?
  Serikali inatoa mkopo wa asilimia ngapi kwa mwanafunzi mmoja?
   
 3. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hivi tumaini ina wanafunzi wangapi?
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wajameni, hivi hiki chuo kina wanafunzi wangapi?
   
 5. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi naona sawa kwani elimu ya chuo kikuu inagharama kubwa katika kuiendesha, mfano wahadhili wanahitaji kulipwa vizuri.
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani Serikali mko wapi Vyuo binafsi wanapandisha ada wanavyotaka huku Serikali imewapunguzia kodi.Wizara ya Elimu mpo?Walalahoi watasoma kweli kwa ada hizi eti kutoka 1.5m to 2.5m asilimia sitini yote kweli.Serikali kupitia Wizara ya Elimu ichukue hatua zifaazo.Jamani wengi ni mashahidi TUMAINI UNIVERSITY imeboresha nini hadi ipandishe ada kiasi hicho.
   
 7. M

  Mukubwa Senior Member

  #7
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 124
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Si vyuoni tu, mbona kuna sekondari ambazo ada yake ni kubwa kuliko ya baadhi ya vyuo? hilo nalo liangaliwe
   
 8. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hicho pekee sio kigezo cha kutumiwa kuongeza ada. Kama ambavyo ada kwenye baadhi ya kindergartens imezidi gharama ya kwenye vyuo - kwa mtazamo wako, una maana ya kusema kwamba kwa kuwa ada ya chuo ni 2.5 million kwa mwaka, basi gharama za kindergaten nazo zisizidi 1 million? Ndicho unachotaka kutuambia au sivyo?

  Tunahoji vigezo vilivyotumika kuongeza ada kwa 60%, kitu ambacho kwa mujibu wa muandishi hapo juu, mkuu wa KKKT ameshindwa kikiweka bayana.

  Imagine mwanafunzi anaingia mwaka wa pili, mzazi wake amefunga mkanda kumpeleka mwanae hapo; ghafla linatokea ongezeko la asilimia 60 kwenye fees. Amwachishe chuo?
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sawa kabisa,lakini kweli wahusika huwa wanasoma malalamiko na ushauri wa JF?
   
 10. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Naona MUHAS na UDOM wakifungua nafasi na kuchukua wadaktari 1000 kila chuo kwa mwaka..basi KCMC, Bugando, HKMU, IMTU watakufa tu..maana serikali wakati ada ni 1.5m private ni zaidi za 5.0 m yaani mara 3 ..yaani hivi vyuo vinapata wanafunzi kupitia Mikopo ili kujitajirisha???

  Tuangalie tu 5 years ..nasema private hawatapata wanafunzi!!

  Je kwa nini TCU isharmonize fees kwa public na private..kwani Bodi ndo hutoa Mikopo???
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli kuna haja kuunda SUMATRA ya ada za vyuo vya Elimu ya juu kama kweli lengo ni kutoa fursa kwa jamii maskini nao wasome.
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Bodi ya mikopo imesema haitafidia ongezeko la ada
   
Loading...