Heparin
Senior Member
- Sep 24, 2021
- 161
- 605
Uamuzi huu umefikiwa na Kamati ya Uongozi Taifa kwenye kikao chake cha tarehe 15 Mei 2024 kwa kuzingatia madaraka yake chini ya Ibara ya 72A(2)(a) ya Katiba ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015 Toleo la Mwaka 2024.
Uamuzi huu umefikiwa kutokana na msimamo wa Chama chetu kuwa baada ya kupitishwa kwa Sheria Mpya ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Mwaka 2024 tunahitaji Tume iliyopo ijiuzulu ili kupata Makamishna wapya na Sekretarieti mpya ya Tume Huru ya Uchaguzi.
Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi inataka Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi wapatikane kwa Watanzania kuomba, kufanyiwa usaili na Rais kupelekewa majina ya kuteua. Makamishna wa Tume wa sasa hawana uhalali kusimamia kuendelea kusimamia uchaguzi huu wa marudio na chaguzi zinazokuja.